UNAVYOTENDA NA KUSEMA NI TAFSIRI YA ULIVYO


 UNAVYOTENDA NA KUSEMA NI TAFSIRI YA ULIVYO 

Bwana Yesu asifiwe Wana wa Mungu
karibu katika siku nyingine na Leo tutaangalia juu ya mtu anavyotambulika mbele Mungu na watu jinsi alivyo ndani yake...

Mathayo 12:33
Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.

Hapa Biblia inatusaidia kuelewa kwamba mtu alivyo ndani anaweza kueleweka kwa kuangalia anavyoonekana nje...
kuonekana nje tunapopasema si umbo au rangi, urefu au ufupi Bali matunda yanayoonekana...

matunda ya mtu yanaonyeshwa na aina ya matendo na maneno ambayo mtu huyatoa..
Yesu alisema mti mzuri utatoa matunda mazuri na mti mbaya matunda yake lazima yawe mabaya na hata siku moja mti mbaya hauwezi kutoka matunda mazuri...

hapa ndipo sehemu ambayo wewe mkristo yafaa Sana upatazame kwasababu hata Mungu huangalia matunda kwa MTU....

Hata Yesu alipokuwa katika kusema Hilo alionyesha kwamba MTU mbaya hawez kuonyesha matunda mazuri ...Bali kile au Ile namna uliyonayo ndani hujidhihirisha nje yenyewe tu...

Mathayo 12:34-35
Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
[35]Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.

ukisoma hapo utaona ansema kuhusu KUNENA au kuzungumza...anatuonyesha ubaya wa mtu ulio ndani huonekana nje pale anapozungumza...
akiwa na maana kuwa Huwezi kuwa na maneno machafu nje halafu ndani ukawa msafi...Bali kinywa Cha MTU kinatoa tafsiri ya Aina ya mazingira yaliyondani ya mtu....na akasema kinywa Cha MTU siku zote hunena kile kilichokuwa ndani ya Mtu huyo...
👉Kama Ni mtu wa masengenyo Basi hayo ndiyo yaliyoujaza moyo
👉Kama ni MTU wa matusi Basi hayo ndiyo yapo ndani ya moyo
👉Kama Ni mtu wa maarifa Basi moyo wako umejaa maarifa kulingana na hekima
👉Kama Ni mtu wa kuzungumza upumbavu tambua moyo wako umejaa hayo

Mithali 15:2
Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; 
Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.

lakini pia matendo yako Ni matunda yanayokueleza kuwa wewe Ni mti gani...na ndiyo maana hata Yesu aliwaita mafarisayo wanafiki kwasababu walikuwa wanaigiza kuonyesha matunda ya wema angali ndani Yao hawana huo wema...

na hata Paulo alisema Hilo kwamba wapo waigizaji wazuri tu ambao utakuta wanamtaja Mungu lakini ukija kwenye matendo Yao Ni tofauti 

Tito 1:16
Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.

lakini Yesu aliweka wazi kwanini wanaigiza wokovu, au wanaigiza kumjua Mungu hao wanafiki ...Ni kwasababu wanataka kutazamwa na watu ili wapate utukufu....

 Mathayo 23:5-7
5 Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
[6]hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi,
[7]na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.

Sasa kumbe unavyoishi na vile unavyozungumza Ni matunda ya nje yanayowakilisha wewe Ni Nani....
kumbuka matendo yako Ni matunda ya aina ya roho iliyo ndani yako...na ndiyo maana hata ukiwa na Roho Mtakatifu Basi matunda au tabia za Roho Mtakatifu zinajidhihirisha nje zenyewe Wala si kuigizwa.....

kaa na Mungu, mtii Yesu kubali kuongozwa na Roho Mtakatifu ndipo utakapoyaonyesha matunda yanayompendeza Mungu....

kumbuka MUNGU ANAHITAJI MATUNDA...

Mungu akubariki

Taifa Teule Ministry
Min.Mathayo Sudai
0744474230/0714732009

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI