MUNGU ANAHITAJI MATUNDA SI KINGINE
MUNGU ANAHITAJI MATUNDA SI KINGINE
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu...
leo Ni siku nyingine ..karibu tujifunze Jambo la msingi Sana kwetu kwa leo, kesho na hata milele yote...
Yohana 15:5
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
hayo ni maneno ya Yesu mwenyewe alipokuwa akisema na watu wake alipokuwa duniani...
👉Alijilinganisha na mzabibu wa kweli halafu sisi Ni matawi ya huo mzabibu. akasema kuwa tawi linapokuwa kwenye mzabibu wa kweli ndipo linauwezo wa kuzaa matunda ya kweli..
👉Sasa mpaka hapo ni lazima ujue kuwa Kama Yesu ndiye mzabaibu na wewe mtoto wake Ni tawi Basi hutoweza kuzaa matunda ya kweli pasipo kuwa ndani ya Yesu mwenyewe...
👉lakini akaaye ndani ya Yes atazaa matuta yanayompendendeza Mungu...
👉atatembea katika utakatifu, na kuwa na haki machoni pa MUNGU..
👉lakini pasipo Yesu sisi hatuwezi kufanya lolote...
ukianza Kuanzia mstari wa kwanza utaona Yesu akitutaka Sana sisi tuwe kwake ili tupate kuzaa matunda...na akasema tawi lisilozaa Mungu mwenyewe atalikata na kulitupa motoni...
KUMBUKA amesema BABA ATALIKATA NA KULITUPA MOTONI..
sasa ukiwa na uwezo wa KUTAMBUA utaona kwamba siyo yeye Yesu ambaye analikata Hilo tawi Bali Ni BABA...
PIA unaweza kujiuliza kwanini kwamba kwanini Mungu analikata tawi Hilo...????
JIBU ni kwasababu halijazaa MATUNDA...
👉Mpaka hapo natamani kanisa la Mungu lijue kuwa Mungu anachokitaza kwetu Ni MATUNDA...
NI HIVI
👉Umefanya Toba ,je unazaa matunda yapasayo Toba??
Mathayo 3:8
[8]Basi zaeni matunda yapasayo toba;
đź‘‹Umeokolewa je unaishi katika haki aliyoikusudia Mungu kwako?
đź‘‹Umri wako wa kukaa kwenye wokovu na Kiwango Cha wokovu wako vinafanan?
đź‘‹Toka umempokea Kristo je Kuna ongezeko la kiroho?
đź‘‹ulivyokuwa hujaokoka na ulivyo Sasa , je Kuna matunda au HAKUNA ?
đź‘‹je unaishi kwenye chuki, kiburi, masengenyo, uasherati, uzinzi , matusi na uovu mwingine Kama ulivyokuwa kabla ya wokovu ??
ZAA MATUNDA ANAYOYATAKA MUNGU BABA...
👉Haijalishi unanena kwa lugha au la ..jua kabisa Mungu hasumbuki na Hilo Bali anaangalia matunda👉Haijalishi wewe Ni Mwalimu mzuri wa Neno kiasi gani, Basi jua Mungu hanashida na Hilo kwako anachohitaji Ni matunda
👉Haijalishi wewe Ni mchungaji , mwimbaji, mwinjilisti, shemasi, mzee wa kanisa n.k, Basi jua Mungu hahangaiki na Hilo kwako Bali anachokitaka Ni matunda..
👉 Mungu anapokupa karama au kipawa fulani si kwamba wewe Ni bora zaidi Bali anataka uwafanye na wengine wazae matunda maana yeye anachokihitaji Ni matunda....
kwasababu yeye Ni MKULIMA..
Yohana 15:1-2
[1]Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
[2]Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
👉MKULIMA huwa anachokitaka shambani kwake Ni MATUNDA ya kile alichokipata na si kingine..
lakini katika hayo yote Ni lazima ujue kuwa hutaweza kuzaa matunda bila kuwa ndani ya Yesu...
đź‘‹Huwezi kutembea katika haki bila kuwa na Yesu
đź‘‹Huwezi kuwa na utakatifu ndani yako bila kuwa na huyu Yesu
đź‘‹Huwezi kuishinda dhambi ya Aina yoyote Ile bila kuwa ndani ya Yesu..
đź‘‹Huwezi kufanya chochote chenye maana mbele za Mungu bila kuwa na huyu YESU...
hiyo yote ni kwasabau wewe Ni tawi tu hivyo Huwezi kuzaa tunda lolote analolitaka Mungu bila kuwa ndani ya mzabibu...
na Kama Huwezi na upo nje ya Yesu Basi jiandae kukatwa na kutupwa nje..
HIVYO
mtii Mungu
muheshimu Mungu
mpokee Yesu
ikatae dhambi
ili uwe imara katika Bwana na uzidi kuzaa matunda
Mungu akubariki sana
Maoni
Chapisha Maoni