USIHANGAIKE NA KIJANA..MUOMBEE


USIHANGAIKE NA KIJANA..MUOMBEE

Bwana Yesu asifiwe mabinti wazuri..

Leo Ni siku nyingine ambapo natamani ufahamu Jambo la msingi kwenye mahusiano...

👉Kuna wengi huwa wanatafuta Sana maarifa na njia mbalimbali za namna ya kufanya mahusiano Yao kuwa mazuri au jinsi ya kuishi na wachumba zao..

👉Hilo si baya tena Ni Jambo la msingi Sana..lakini Kuna jambo la msingi kabla ya hayo yote..nalo Ni maombi....

Hebu Soma hapa👇

1 Timotheo 2:1

[1]Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

Hayo Ni maneno ya mtume Paulo alipokuwa anazungumza na kijanaTimotheo ambaye alikuwa anaanza huduma...

unaweza kujiuliza kwanini hakumwambia maarifa kwanza au hekima kwanza, au kuhubiri sana

👉lakini utagundua kumbe Mambo yote ambayo tunayapata kutoka kwa Mungu huwa yanafanya kazi sawasawa pale tunapokuwa waombaji..

na ndiyo maana Paulo alitulia neno KWANZA..yaani lifanyike kabla ya mengine..

👉kumuombea mchumba Ni Jambo la msingi kabla ya Mambo mengine yote unayoyataka ..

đź‘‹ukimuombea unamlinda

đź‘‹ukimuombea unamuhifadhi mbali na vishawishi 

đź‘‹ukimuombea unasababisha kufanikisha Yale yanayotakiwa kumfikisha kwenye ndoa

đź‘‹unapomuombea unamfanya kupenda na kumuheshimu

đź‘‹ukimuombea unaileta amani kwenye maisha yenu ya uchumba hata baada ya ndoa..


ukiwa na maarifa ya NDOA na usiiombee ndoa ..Basi jua HAKUNA litakalofanyika..Bali maarifa hayo yatakuwa na maana na kutenda kazi kwelikweli baada ya kuwa Kuna maombi nyuma yake...

Maombi huwa yanaiandaa kesho yako pasipo kujua ..unapoomba Maombi yako yanaiendea Hadi kesho yako...na utashangaa unachokishughulikia Leo kwenye maombi..unakikuta kesho, kwasababu maombi huwa hayaishii inaposema AMINA Bali huitengeneza kesho yako ( wakati ujao )

👉Kama wewe Ni Binti ambaye hujaolewa bado, Basi usijaribu kupuuzia maombi hata Mara moja..

👉usikubali kuambiwa na sauti yoyote ya kumwambia  maombi hayasaidii kitu kwenye ndoa..Bali tambua kuwa maombi hayashindwi kitu..

👉Kuna wakati unaweza kumuona mwenzako, mchumba haeleweki kabisa..kila utakachomwambia anaonekana haeleweki kabisa..

Basi leo Anza kuingia kwenye maombi huko ndiko kwenye majibu yako..USILIE!!

Pia usiwe Kama mwanamke mjinga asiyejua ambaye ukimkuta Ni mjuaji  na  muongeaji kweli lakini sirini anateswa na mahusiano....

 Mithali 9:13

Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.

KUMBUKA Shetani hapendi uolewe.. hivyo jua upo kwenye Vita na njia ya Vita Ni kumuombea mchumba vizuri..UTAMWONA MUNGU AKIMWAIDIA NA KUMTETEA..

MUNGU AKUBARIKI


laddies in Christ

Mwl/Ev. Mathayo Sudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI