MTII MUMEO KAMA KANISA LINAVYO MTII KRISTO
MTII MUMEO KAMA KANISA LINAVYO MTII KRISTO Bwana Yesu asifiwe watoto wa Mungu, Leo naomba kuwakumbusha au kuwajulisha jambo la muhimu lenye kuleta ustawi ndani ya nyumba. Kwanza naomba kukueleza kuwa ustawi wa nyumba unategemea sana aina ya mke aliyepo ndani ya familia hiyo, Leo naomba nkujulishe mambo fulani kutoka kwenye mistari hii ya Biblia👇 Waefeso 5:22-24 [22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. [23]Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. [ 24]Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Hapo kuna jambo la ajabu na lakushangaza, limesemwa kwa habari ya mwanamke kumtii mumewe. Hebu soma mstari wa 22 " Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu " Biblia inaeleza kuwa mwanamke anatakiwa amtii mume wake kama vile anavyomtii Yesu Kristo, yaani kama vile mwanamke aliyeokoka anavyomtii Mungu basi n...