FUNGA UDHAIFU WAKO KAMA MWANAMKE






Bwana Yesu asifiwe mabinti wote ndani ya Darasa hili.ninawasalimu kwa jina safi la Yesu Kristo


Awali ya yote nichukue nafasi hii kukushukuru wewe uliyechukua hatua ya kusoma ujumbe huu.

      Kama binti na mwanamke unayejiandaa kuwa na familia ni lazima uwe na desturi ya kujiuliza maswali kadhaa kama haya;


1: Udhaifu wangu ni upi?

2: Nina vigezo vya kunifanya nifikie kile ninachokitaka?

3:Mambo gani ya kuyaacha ili ku wangu?

4:Asili ya udhaifu wangu ni nini?


Desturi ya Mwanamke kujiuliza maswali kama hayo na mengine mengi kwenye maisha yako, itakufanya kuishi maisha ambayo yana kibali mbele za Mungu kwani utakuwa ni mtu wa kufuta kila aina ya udhaifu na changamoto itakayoamka ili kukuzuia katika safari yako, kwasababu hakuna mtu duniani awezaye kuchukua hatua ya kitu asichokijua, maana ni wengi wenye kuishi na udhaifu bili kujua ni udhaifu.



👉Kwanza ni lazima ufahamu kwamba  kila kitu kinachokuzunguka chenye asili ya dunia hii mbovu kinakiri kuwa mwanamke ni dhaifu, na vingine vinahitaji kukuangusha kupitia udhaifu vinauona kwako.

        

   Mifano kutoka kwa watu wa dunia hii

1.In every cry there is a woman behind

2.No woman, no cry. Na mingine mingi ambayo huonekana kuwa ni kawaida lakini ina  nguvu ya kumweka mwanamke chini siku zote.


Sasa wewe kama binti ni lazima ufahamu hatua sahihi za kuchukua ili kuufunga udhaifu wako unaokutesa


Hebu tuyachunguze maandiko kidogo:


MWANZO 3:1-5

[1]Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?

[2]Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;

[3]lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.

[4]Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

[5]kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.


Hebu tazama jinsi mwanamke alivyofanywa mateka na shetani katika bustani ya Edeni.


Swali ambalo shetani alimuuliza mwanamke ni moja tu kwamba ATI! HIVI NDIVYO ALIVYOSEMA MUNGU, MSILE MATUNDA YA MITI YOTE YA BUSTANI?


Sasa ukitazama vizuri jinsi shetani alivyouliza utagundua kwamba shetani alikuwa anajua kwamba Mungu amezungumza na mwanadamu kuhusu utaratibu wa kula matunda ya bustanini, 

na pia shetani moja kwa moja aliomuonyesha mwanamke kuwa kile anachomuuliza, yeye mwenyewe anakipinga na ndiyo maana akasema ATI! .kama sivyo basi shetani angesema Kwa namna nyingine.

     

  Na hapa pakusaidie kutambua kama mwanamke ni lazima ujihadhari na mtu ambaye anakuuliza habari ya jambo ambalo analijua katika maisha yako ya kiroho.

Ukiona mtu anakuuliza jambo nyeti ambalo analijua, basi anza kuwa na mashaka naye, ni lazima nyuma yake kuna ajenda mpya


Mwanamke Eva alichokosea ni kumwambia shetani madhara ya kula tunda, Na ndipo shetani alipopata upenyo wa kujifanya mwema.


Soma hapa

[3]lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, MSIJE MKAFA


Kitendo cha kuzungumza kuhusu kufa baada ya kula tunda, shetani akadakia na kusema Hakika hamtakufa

Kwa maana nyingine, shetani alianza kutafuta namna ya kumuhakikishia Eva kwamba Mungu ni muongo na kwamba lengo la kuwanyima ni kuwazuia waziwe kama yeye na si kifo.


Jambo hili limekuwa tatizo kwa mabinti wengi jambo linalopelekea kukosea, kwa kuiacha njia sahihi na kwenda kusiko sahihi kwasababu wengi wamesikia sauti ya Mungu lakini baadae wanaisikiliza sauti ya shetani.


MFANO🖐️

Binti umeambiwa na Mungu kwamba Mume wako ni mtumishi wa Mungu, baadae baada ya kutambua kuwa huyo mume ana maisha duni, hatoweza kukupa kila unachokitaka, unaanza kumtamani mtu mwingine labda mfanya biashara kwa tamaa ya uhai wa kimwili na pesa.

Jambo moja ni lazima utambue,

  

     Mungu anapomtuma mtu kufanya jambo anatambua usalama atakaokuwa nao, pia Mungu humualifu mwanadamu habari ya kila aina iliyoandiliwa. AMOSI 3:7, Matendo ya mitume 22:17-19


              

                       MABINTI HUKOSEA WAPI.?

Mabinti wengi katika maisha ya leo huuruhusu udhaifu juu ya maisha yao na hata kujitia matatizoni


1:Kukosa uvumilivu

    

Ni lazima binti utambue kwanza kuvumilia ni ishara ya mtu mwenye roho mtakatifu. Wagalatia 5:22-23

Ukiona umekosa kuwa na uvumilivu katika mambo unayopitia au uliyoyakusudia jua na tambua unaweza kuwa umepungukiwa katika mambo yote maana roho nj yuleyule ampaye mtu kuvumilia.

      Mabinti wengi, ukimuuliza anachokiwaza sasaivi atakwambia, anataka kuulowa, umri wake ni miaka ishirini tu na anasema amechoka kuomba na kusubiri.

Biblia inasema, Waebrania 6:12

[12]ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.

Ukishindwa kuvumilia katika mambo yako tambua shetani atatumia kile kinachoitwa udhaifu kwako na hata kukuletea watu wasio sahihi


2: Kukosa Nguvu ya Maombi


Katika ulimwengu wa Roho tumehaidiwa baraka za kila aina

           Waefeso 1:3

[3]Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;

Sasa watu wengi hujidanganya wenyew kuwa wamebarikiwa katika vyote na wanauwezo wa kufanya chochote, bila hata maombi,....UMEDANGANYWA NA UNAJIDANGANYA.

Biblia inasema ametubarikia baraka zote ZA ROHONI katika ULIMWENGU WA ROHO. sasa ili uzipate baraka zote hizo ni lazima uwe wa ufungua wa kufungulia chumba cha baraka hizo KATIKA ULIMWENGU WA ROHO. Si tu baraka eti kisa umeokaka,,,HAPANA!. Ni lazima uwe na nvuvu ya maombi ambayo ndiyo ufunguo wa chumba hicho, sasa uskikae kama wasichana wa dunia hii ni lazima uwe mwombaji.


3: Kuiga mambo yasiyofaa


Jambo hili linashida sana, kama binti ulkyeokoka ni lazima utambue kwamba kila kitu kinachoingizwa kwenye dunia ya leo, chenye kupendeza kwa macho ya nyama. Kinalenga kukuingizia udhaifu wa kukuangusha.

   Sasa wako mabinti wengi wamekwepana na mkono wa Mungu kwasababu wamefuatisha mambo ya dunia hii.

            Tambua kwamba mahali popote palipo na Mungu ni lazima pawe na utakatifu, na mambo yote ya dunia yasiyompendeza Mungu,ndiyo yanayopoteza utakatifu. Basi ni lazima uwe makini unpoishi katika dunia hii iliyojaa dhuluma na udhalimu.


4: kuwa na tamaa kubwa ya ndoa 


Mabinti waliookoka ni lazima wasiwe na desturi ya kuonyesha haja yao ya kuwa na familia, kwasababu utakapoonyesha tu, shetani ataanza kukutamanisha mambo yaliyopo kwenye ndoa, utajikuta umekurupuka tu na kuingia kwenye ndoa isiyo sahihi kabisa. Tambua kuwa unapokuwa katika hali hiyo unampa adui nafasi na hata wanaume wanakuona katika kiwango cha chini.

   Utakuta binti anaposti kwenye status NATAFUTUTA MUME, mara ,NIKO SINGLE mara anajiposti akiwa na mavazi ya ajabu akijua atapata mume kumbe hajua anaipoteza thamani yake na wanaomtamani ni wale wasio na hekima mwisho wa siku anaolewa na kuanza kujuta. Siku zote usijaribu kuionyesha jamii kuwa unahaja na mume maana itakushusha thamani ,wewe mtazame na mlilie Mungu tu kwenye haja yako na BWANA ATAKUINUA ZAIDI.

Kuwa kama mashujaa wa kibiblia.


          MUNGU AKUBARIKI SANA,!

  0655891197, 0628187291,,0744474230 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI