WALIO NDANI YA NDOA WANATAMANI KUTOKA NA WALIO NJE HUTAMANI KUINGIA.

WALIO NDANI YA NDOA WANATAMANI KUTOKA NA WALIO NJE HUTAMANI KUINGIA.

Maana yake nini na ni kwanini pia nini kifanyike? 

Bwana Yesu asifiwe watoto wa Mungu. 

Ni mara nyingi sana tumekutana na watu wanaozungumza kauli hii, kwamba ndoa ni fumbo kwasababu waliopo ndani ya ndoa wanatamani kutoka na waliopo nje wanatamani kuingia, 

   Maana ya jambo hili ni nini na sababu yake ni nini,? 

Kama mtu unayetarajia kuingia kwenye ndoa ni lazima ujue jambo hili ili usije ukaingia alafu na wewe ukatamani kutoka. 

Mimi ni Mathayo Sudai karibu sana🙏

WALIO NJE WANATAMANI KUINGIA. 

Hii inasimama kuwakilisha wale wote ambao bado hawajaolewa, ambao mara nyingi ukiwaulizaa hata haja walizonazo kwenye maombi yao basi watakwambia kumpata mwenza ni moja ya maombi yao. Huzunguka na kuhangaika ili tu haja yao itimie. 

  Kimsingi si kitu kibaya na ndiyo maana hata Biblia inasema👇

Mwanzo 2:21-24

[21]BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

[22]na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

[24]Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.


WALIO NDANI WANATAMANI KUTOKA 

Hawa ni wale ambao wapo ndani ya ndoa tayari na wanatamani hata wangekuwa hawajaolewa au kuoa, hawa huona maisha ya pekeyako ni bora kuliko ya kuolewa yaani wamechoka sana maisha ya ndoa 

  Wanaishia kutamani tu kutoka lakini hawawezi, kwanini hawawezi? 

Soma hapa 👇

Mathayo 19:9

[9]Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Marko 10:11-12

[11]Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;

[12]na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.


Luka 16:18

[18]Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.


Unaona👆 hapo utakuta watu walioana ndoa takatifu, na wanajua wakiachana na kuoa tena wanazini

Kwahiyo wanaishia tu kutamani kutoka nje lakini ndoivo tena hawawezi na wanaishia kuishi kwa maumivu tu kila siku mwisho wa siku wanajitia kwenye hatari mbaya kama kujinyonga, kunywa sumu na vitu vingine vya hatari

Sasa utaona walitamani wenyewe kuingia humo halafu wanaishia kulia na kutamani kutoka, SHIDA NINI? 

Tatizo kubwa ni MATARAJIO

Kivipi? 

Watu wengi huingia kwenye ndoa kichwakichwa wakiwa na matarajio yao, kwamba watakapoingia watakutana na kitu hiki, hiki na hiki. 

Unapoweka matarajio ya kitu kwenye ndoa, ni lazima ujue yule mwenzako anafikra zake na akili yake. 

Unaweza kutarajia kuwa utakutana na kitu fulani, alafu ukakikosa basi majuto yanaanza

Pale ambapo utaanza kuona mwenzako anakuletea na kufanya mambo ambayo hata hukuwahi kuyawaza hapi ni lazima utajua kuwa ulichokifuata kwenye ndoa umekikosa. Na unajua nini kitafuata


Soma hapa👇

Mithali 13:12

[12]Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. 

Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.

  Kwahiyo unaweza ukajiukiza nifanye nini sasa kama nj ivo? 

Unapojiandaa kuingia kwenye ndoa, usiweke matarajio ya kitu fulani kwa asilimia zote. 

Jambo unatakiwa kulifanya ni kujitesa sana katika maombi ili yule mchumba wako awekwe katika namna sahihi ya kumpendeza Mungu Lakini kuipendeza ndoa yenu. 

  Kila kitu utakachokutana nacho kwenye ndoa yako, hakiji tu eti kwasababu kipo ila kunakuja kwasababu umekiandaa mwenyewe kwenye kipindi cha uchumba. 

Kipindi cha uchumba siyo kipindi cha wewe kushinda kwenye kioo, kutwa kujitazama uzuri wako ulionao na kujilinganisha na wengine

Kipindi cha uchumba si kipindi cha kulegea kuona kama umepata tayari 

Kipindi cha uchumba si kipindi cha binti aliyeokoka kuishi kama mtu ambaye hajakombolewa hajui cha kufanya. 

Bali kipindi hiki cha uchumba ni kipindi cha wewe kuomba sana iki ikipande unachotaka kukivuna kwenye ndoa kwasababu uimara wa ndoa hauanzi pale unapoolewa bali kabla ya kuolewa. 


Maandalizi ya ndoa yako usiyafanye kimwili kwa kujiwekea matarajio ambayo yasiyohusiana na Mungu kwasababu kuna hatari sana pale ambapo utakuta kile ulichokitarajia hakipo, 

  Utaanza kuingia kwenye majuto na utaona umechoka ghafla na unatamani kutoka ila haiwezekani. Na hiki ndicho kinawakuta wengi walioolewa na waliooa sasa hivi yaani wengi wao wanajuta. 

Kwasababu👇

Mithali 16:1

[1]Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; 

Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.


Sasa kama jawabu linatoka kwa Bwana, inafaa sana ukijiweka vizuri na Bwana kwani yeye ndiye mwenye jibu la mwisho. 

Mungu akubariki sana na kukuponya kwa jina la Yesu. 


Taifa Teule Ministry 

Minister Mathayo Sudai 

0744474230 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI