MTII MUMEO KAMA KANISA LINAVYO MTII KRISTO


MTII MUMEO KAMA KANISA LINAVYO MTII KRISTO 

Bwana Yesu asifiwe watoto wa Mungu, 

Leo naomba kuwakumbusha au kuwajulisha jambo la muhimu lenye kuleta ustawi ndani ya nyumba. 

Kwanza naomba kukueleza kuwa ustawi wa nyumba unategemea sana aina ya mke aliyepo ndani ya familia hiyo, 

Leo naomba nkujulishe mambo fulani kutoka kwenye mistari hii ya Biblia👇


Waefeso 5:22-24

[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

[23]Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.[

24]Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

   Hapo kuna jambo la ajabu na lakushangaza, limesemwa kwa habari ya mwanamke kumtii mumewe.


Hebu soma mstari wa 22

  "Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu

Biblia inaeleza kuwa mwanamke anatakiwa amtii mume wake kama vile anavyomtii Yesu Kristo, yaani kama vile mwanamke aliyeokoka anavyomtii Mungu basi ndivyo mke anavyotakiwa kumtii mumewe.

Soma hapa👇

1 Petro 3:6

[6]Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.

Mwanamke sara alimtii sana mumewe Ibrahimu mpaka akamwita, Bwana. Hebu jiulize ni nidhamu ya namna gani mpaka mke anamwita mumewe Bwana,. 

Yaani heshima yake inafanana na vile anavyomtii Kristo. Au mke anamuheshimu mumewe hadi anamwita Baba na ndivyo wanawake wanatakiwa kuwatii waume zao, 

👉Kwa namna hii mwanamke utaepusha mambo mengi ambayo shetani pengine angeyaingiza kwenye familia yako

Kwa mwanaume aliyeokoka na kupokea heshima ya namna hii kutoka kwa mkewe basi tambua shetani atakaa nje ya familia bila kupata nafasi.

👉 Na hii ndiyo raha ya ajabu wanayoipata watu wanaooana wakiwa wameokoka wote wawili- yani kumkosesha shetani nafasi ndani ya nyumba. 

 Hata kama ikatokea siku mmekosa chakula, mwanamke usijaribu kuishusha heshima yako kwa mumeo utamkaribisha shetani kama wafanyao wanawake wa dunia hii ambao Ayubu anawaita wapumbavu

Ayubu 2:10

[10]Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.

Unaona kumbe ukiona mwanamke anashusha heshima yake na kuanza kumdharau mumewe na kutamani kuachana naye basi jua huyo mwanamke ni mmoja wa wanawake wapumbavu wa dunia hii, ambao utakuta wanasema maneno kama haya👇

👏Mimi mume aliyeishiwa pesa simtaki

👏Mwanaume ni pesa 

👏Mwanaume bila pesa utawaita wasichana wote dada

Haya ni baadhi ya maneno ya wanawake wapumbavu wa dunia hii wasiotaka kuona wanaume wakiishiwa au kukosa pesa huku wakishindwa kujua kuwa kuna mwanaume mmoja mcha Mungu aliyeitwa Ayubu ambaye aliishiwa vyote, si mali tu bali mpaka afya na baadae akafanikiwa kwa kiwango cha ajabu kwasababu, kuishiwa kule kulikuwa ni daraja la kupata vingi. 

  " BINTI UKIWA KWENYE NDOA MTII MUMEO" 


KUMBUKA

Biblia inasema, mtii mume kama unavyomtii Yesu Kristo, hebu jiulize kidogo👇

Ni mara ngagi umemuomba Mungu kitu na bado hajakujibu? 

Au ni mara ngapi umeomba kupata mume bora lakini bado hujampata? 

   Pengine ni mara nyingi,! 

Je! Ulipoona Mungu hajakujibu bado, ulimdharau? Au ulitaka kuacha wokovu? 

Jibu pengine ni hapana! 

   Kwa nini hujaacha wokovu au kwanini hujamdharau Mungu? 

Hujafanya hivyo kwasababu unajua ulichokiomba Mungu anakiandaa, bado anaandaa mazingira ya wewe kukipata na yakishakaa vizuri utakipata. 

  Nikupe siri moja binti,  hata haya masomo unayoyasoma kila siku kuhusu ndoa, ni maandalizi ya mazingira ambayo Mungu anayafanya ili utoshe kuwa na ufahamu wa kuishi ndani ya ndoa. Usije ukajaribu kupuuzia maana utachelewesha mazingira ya kuipokea ndoa yako. 

  Si hapa tu lakini jitahidi sana kutafuta maarifa ya ndoa kama unamuomba Mungu akupe ndoa takatifu. 

Kwasababu akikupa bila kuwa na ufahamu mzuri basi jua unaweza kuishia pabaya. 

Ni sawa na mtu kuomba anunuliwe gari wakati hawezi kuendesha, unafikiri akilipata gari na huku hajui kuendesha nini kitatokea? - - ajari na hata kifo


..... Tuendelee.... 

Sasa kwanini kwa mume ushindwe kufahamu kwamba kukosa kipato, chakula na mali ni kwa muda tu kuna wakati mtapata? Kama kwa Mungu unaweza kujua hayo.?


Lakini tukiangalia mstari wa 24 anasema 👇

[24]Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

Ametoa tena namna nyingine kuwa kama vile Kanisa yaani watu waliookoka wanavomtii Bwana vivyo hivyo mke anapaswa kumtii mumewe katika yote

Sasa kuna mambo ambayo kanisa hufanya na litaendelea kufanya kila siku kwasababu linamtii Kristo, mfano👇, 


1. Kanisa litamsifu Kristo

   Sasa kwasababu kanisa linamtii na kumuheshimu Kristo ni lazima na huwa linamsifu Yesu kwa matendo makuu, kwa upendo wake, kwa vyote pia

Na wewe mwanamke kwasababu unatakiwa kumtii mume kama kanisa linavyomtii Yesu, basi huna budi kumsifu mume wako pia. 

Kivipi? 

Mume anaweza kutoka kazini amechoka, wewe unatakiwa umsifu kwa jitihada zake za kila siku kuendesha familia. 

    Lakini kuna wanawake ambao wakiona mume amerudi kutoka kazini baada ya kumkaribisha tu utasikia umetuletea nini kutoka huko utokako! 

Yaani wao wanafikiri kila siku ni kupata tu hawafikirii kukosa, 😯 hiyo ni mbaya sana maana kama ikitokea amekosa hali ya hewa inaweza ikabadilika kabisa hapo ndani. 

  Kumbe ni lazima baada ya kumkaribisha, mwambie "pole na hongera pia kwa majukumu babaangu" na maneno fulani ya kumsifia bila kujua kapata au kakosa, halafu kisha mengine atakushirikisha baadae mkiwa ndani wenyewe. CHUKUA HII ITAKUSAIDIA. 


2. Kanisa litampenda Kristo kwa nguvu zote, akiri/moyo wote na kwa Roho yote

Hebu soma hapa👇

Kumbukumbu la Torati 6:5

[5]Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.


👉Unajua mke amepewa jukumu la kuifanya nyumba ijawe na upendo mkuu,

   Mume anapompenda mkewe kinachotokea ni kwamba naye mke atampenda zaidi. Na ndiyo maana Biblia inasema mume anayempenda mkewe amejipenda mwenyewe kwasababu upendo wake utarudisha majibu ya kupendwa zaidi na mkewe 

Kama vile kanisa basi yafaa sana mke nawe awe hivyo kwa mumewe. 

  Kuna familia ambazo upendo haupo kabisa, wanaishi kwa maumivu, hawana furaha na matatizo mengi yanawakumba. 

Biblia inasema upendo haushindwi kitu, yaani ni kwamba😁

👉Hakuna mlima mrefu ambao upendo hauwezi kupanda

👉Hakuna moto mkubwa ambao upendo hauwezi kuuzima

👉Hakuna hasira ambayo upendo hauwezi kuishusha

👉Hakuna barafu ngumu ambayo upendo hauwezi kuiyeyesha

👉Hakuna tatizo kubwa ambalo upendo hauwezi kulitatua. 

Hebu soma hapa👇

1 Wakorintho 13:8

[8]Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

"UPENDO HAUSHINDWI KITU"

Njia ya kumaliza kelele ndani ya ndoa ni upendo wa kweli unaoambatana na matendo ya upole na moyo wa utulivu. 

  Kwa mambo hayo tu utashaangaa hata mume ambaye ni msumbufu anatulia, huo ni muujiza uliopo ndani ya upendo. 

Hebu soma hapa👇

1 Petro 3:1

[1]Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;


3. Kanisa litamfuata Yesu na kuwa chini ya uongozi wake

Mungu akikupa mume basi ni lazima utambue kuwa amepewa agizo la kukufikisha ng'ambo pamoja naye, katika huduma, hata maisha ya kawaida. 

Mume aliyeokoka huwa hana uwezo wa kuipoteza familia yake, lazima aitunze familia yake pia huku akipata mwongozo kwa Kristo jinsi ya kuendesha maisha kwa utaratibu chini ya nguvu za Mungu. 

Wengi mnaweza kusema,,, "mbona wanaume wengi wa makanisani huwa ndiyo wana tabia za ajabu kuwasumbua wake zao"? 

👏Kuna tofauti ya mtu aliyeokoka na mtu anayeingia kanisani, kuna vijana wa ajabu wanaweza kuwa wanaingia kanisani kila siku ila hawajaokoka sasa wewe ukienda kichwakichwa utakosea na mwisho wa siku kulitukanisha jina la Yesu, 

Kuwa makini na ndiyo maana huwa nasema omba sana🙏

Lakini Biblia inasema mwanamke atamfuata mumewe na atapata mwongozo kutoka kwa mumewe kama vile kanisa linavyomfuata na kupata mwongozo kutoka kwa Kristo. 

Kuna wanawake ambao wanaishi utafikiri wao ndiyo wanaume,

  Yani

👏 utakuta mwanamke amejawa na huruka hata kwa asichokijua

 👏Utakuta mwanamke anamuendesha mumewe utadhani yeye ndiye amemuoa


👏Ni muongeaji mjuaji wa kila kitu, hataki hata kumsikiliza mumewe, jambo ambalo linawafanya wanawake wengi kushindwa kujua mapenzi ya Mungu ndani ya familia zao. 

Binti lazima ujifunze kuwa si mke tu bali mke mwema 

  Tabia ya kanisa kwa Kristo ndiyo iwe tabia yako kwa mumeo, na Mungu atakuwa pamoja na wewe kwa jina la Yesu. 

Mungu akubariki sana



Taifa Teule Ministry 

Mwl/Ev. Mathayo Sudai 

0744474230 / 0628187291 





  



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI