TABIA MBAYA ZA WASICHANA KWA WACHUMBAWAO NA WENGI ZINAWAGHARIMU

 TABIA MBAYA ZA WASICHANA KWA WACHUMBA WAO NA WENGI ZINAWAGHARIMU

Bwana Yesu asifiwe mabinti wa kristo, karibu katika ujumbe huu ambao una mambo ambayo huwa yanawafanya wanawake wengi kushindwa kuishi kwa uhakika ndani ya ndoa zao na hata wengine kushindwa kuolewa.👇

Hizi ni tabia unazostahili kujitahidi sana kuziepuka kwa namna yoyote ili kuijenga ndoa imara na thabiti

   Mimi ni Mwl Sudai karibu sana👇


1.KUWA MUONGEAJI SANA


   Watu wengi katika maisha wanashindwa kutofautisha kati ya ucheshi na uongeaji mwingi. Mwanamke anapokuwa muongeaji sana mbele za mume wake/mchumba wake basi ni lazima atambue kuwa ni jambo ambalo si salama.

Unaweka ukakuta mwanamke anakushushia story za watu wengine wengi mpaka unashangaa kwamba ameyajuaje hayo yote, yani kila unachomwambia yeye anajua. Sasa hiyo ni mbaya sana na ndiyo maana hana hata Biblia inasema mwanamke awe mstahivu na mtulivu. Mwanamke jitahidi usiwe mwongeaji sanaaa mbele ya Mume au mchumba, jitahidi kumuonyesha kuwa hujui na unatamani kujua kutoka kwake kwasababu wanaume hupenda kuonekana wanajua kuliko mwanamke


2. KUTOKUTULIA NYUMBANI


Hili jambo ni msingi imara sana kwa wanaume wengi pale wanapoamua kutafuta mke.

  Binafi nimefanya utafiti kwa vijana wengi wanaoongelea kuhusu habari za kuoa nikagundua asilimia kubwa sana wanapenda kuoa mke asiye na kazi wakidai kuwa wenye kazi hawawezi kuwalelea watoto. 👇


Hii ni imani dhaifu sana iliyopo katika akili za vijana wengi.

Hebu soma hapa👇


Mithali 31:10-14

[10]Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? 

Maana kima chake chapita kima cha marijani.

[11]Moyo wa mumewe humwamini, 

Wala hatakosa kupata mapato.

[12]Humtendea mema wala si mabaya, 

Siku zote za maisha yake.

[13]Hutafuta sufu na kitani; 

Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.

[14]Afanana na merikebu za biashara; 

Huleta chakula chake kutoka mbali.


Unaona kumbe mke hutakiwa kuwa anajishughulisha na kazi ili kuongeza kipato tena Biblia inamwita mke huyu ni mke mwema,👇

Sasa utajiuliza vipi kuhusu kulea watoto? 

Soma mstari huu👇

Mithali 31:15

[15]Tena huamka, kabla haujaisha usiku; 

Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; 

Na wajakazi wake sehemu zao.


Kumbe mke huyu huandaa kila kitu kabla ya majukumu yake lakini pia ni lazima mwanamke ajue kuitunza familia pale tu anapokuwa huru, free. Ni lazima ajue kuwalea watoto wake pia. 


Sasa usiogope hata kama una kazi au huna panga mambo yako vizuri ili uhakikishe unakuwa na muda wa kukaa na familia. 

👉👉Lakini wanawake wengi hukosea pale wanapokuwa wanatumia muda mwingi kuwatembelea mashoga zake bila kujua kuwa kuna wakati anatakiwa kuwa nyumbani, kukaa na mume au familia yake. 

👉👉 Binti jifunze kuwa muda mwingi unatakiwa kuwa na familia yako kuliko marafiki zako


3.KUCHUKUA MAMLAKA YA MWANAUME

  Kuna wanawake ambao ukiwakuta ndani ya nyumbe unaweza kufikiri wao ndo wanaume, wanaishi kwa amri, yani wanataka kila watakachosema basi kiwe ndio, na wengine wamefika mbali hata kuwaendesha waume zao. 

👉Yani unaweza kukuta mwanamke anamuendesha mumewe mpaka unamuinea huruma mume. 

   Lakini kumbuka Biblia inavyosema


Mwanzo 3:16

[16]Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.


Mwanamke ni lazima awe na dalili ya kumilikiwa yaani kuwa chini ya mume


Soma hapa pia👇


1 Wakorintho 11:10

[10]Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.


4. LAWAMA NYINGI

Hili ni jambo ambalo wanaume wengi hulichukia, 

Unakuta mchumba hajakutafuta  kidogo binti anamtafuta na kuanza kumpa lawama bila hata kujua sababu. 

👉Mwanaume ameshindwa kufika kwenye birthday yako inakuwa vita bila kujua sababu. 

Ni lazima binti uwe mpole mpe salamu kwanza mchumbaako baada ya hapo ndipo muulize.... 

Mfano👇

Mchumbaangu mzuri mbona leo hujanitafuta kabisa shida nini au ulikuwa na majukumu mengi sana mchumbaangu? 

Au leo sijakuona kwenye birthday yangu kabisa na si kawaida yako vipi mume wangu kulikuwa na shida gani babaangu? 

đź‘ŹHapo unamjengea kujua kuwa unamuheshimu hata kama kakosea, na kama kweli kakosea kwa utangulizi huo tu mzuri wenye nidhamu basi anakuwa mpole. 

   Lakini ukianza tu mara oo mbona hujanitafuta, mara mbona sikuelewi sikuhizi mara ooh mbona unanifanyia ivo. Bila hata salamu. Basi binti nakupa pole na jiandae kuwapoteza wengi. 


5. KUWA NA MARAFIKI WA KIUME ZAIDI KULIKO WANAWAKE

Moja ya vitu vinavyoleta matatizo kwenye uchumba wa watu wengi ei pale ambapo mchumba anakuwa marafiki wa jinsia tofauti na yake zaidi kuliko wa jinsia yake. 

👉Ni lazima maswali yataamka na kiasi cha uaminifu kitapungua kwa mwanaume au hata mwanamke. 

Utakuta una mchumba af yeye anamarafiki wa kike wengi na anamazoea nao sana. Jambo utakaloanza kulifikiri ni nini kipo kati yao. 

Vivyo hivyo hata wanaume huwa hawapendi mke au mchumba mwenye marafiki wa kiume zaidi kuliko wanawake wenzake maana ni lazima akujengee maswali hata kama umeokoka


   Hivyo basi ili kulinda uhusiano ulionao na mchumba wako basi ni lazima ujue vitu ambavyo ukivifanya basi vinaweza kuhatarisha uchumba wenu. 

Jitahidi kuiga mifano ya wanawake wa kimungu wa zamani ambao waliwapendeza waume zao pamoja na Mungu. 


Soma hapa👇👇

1 Petro 3:3-6

[3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

[4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

[5]Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

[6]Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.


Mungu akubariki sana 

Mwl /Ev. Mathayo Sudai 

Taifa Teule Ministry 




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI