JINSI YA KUJITENGA NA IMANI
JINSI YA KUJITENGA NA IMANI Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, karibu katika kipindi cha ASUBUHI morning glory ambapo kutakuwa na Maelezo lakini pia sauti ,voice note kwa ufahamu zaidi. Yuda 1:3-4 [ 3]Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. [4]Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Hpo tunaona Maelezo ya Yuda kuhusu kulionya kanisa juu ya kuishi ndani imani Kumbuka imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo, (Warumi 10:17 ) Kwahiyo imani yetu kwa Mungu inakuja pale tunapolisikia neno la Mungu la kweli na kukitii. 👉Lakini ukilisikia pasipo kutii maana yake halijengi imani yoyote kwako 👉Au kama umeliasi neno la...