SOMA BIBLIA UJUE HAYA👇
SOMA BIBLIA UJUE HAYA👇
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu.
Leo ni siku nyingine, naomba tutazame jambo moja lenye msingi sana mbele za Mungu kwa faida yetu wenyewe.
NA Hili ni kuhusu usimaji wa Biblia.
👉Biblia kwa wakristo Wengi imekuwa kama ni kitu kisichokuwa na thamani
👉Imekuwa kama kitu cha kawaida tu
👉Biblia imekuwa kama vile ni kitabu kama vitqbu vingine.
👉Wengi wetu husoma vitabu lakini siyo biblia
Bila kujua kwamba Biblia ndicho kitabu cha ajabu kuliko vitabu vyote...Haleluyaa.
👉Biblia ndicho kitabu pekee kilichobeba siri ambazo hazipo kwenye kitabu chochote duniani
👉Biblia ni kitabu pekee ambacho kimebeba jibu la kila swali alilonalo mtu
👉Biblia ndicho kitabu ambacho kimejaa suluhu kwa kile kinachowatesa watu ulimwengini kote.
Lakini cha kutisha zaidi kuhusu biblia ni kwamba ndicho kitabu pekee ambacho kimebeba siri za aliyeumba mbingu na nchi
đź‘ŹKimebeba siri za mwokozi ambaye hakuna mwenye upendo kama yeye kwasababu ya kile alichokifanya cha kukubali kufa kwaajili ya wengine wapone..YESU KRISTO MFALME
NA ndiyo maana Mungu mwenyewe anataka watu wake tukisome, tayashike ya humo ndipo atubariki na kufanikiwa zaidi
Yoshua 1:8
[8]Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Boblia itakufanya kimjua aliyekuweka hapo
Biblia itakufanya kujua kinachokutesa na pia itakupa jibu lako.
Kama wewe ni MKRISTO na unampenda Mungu,...kwanini hutaki kukishika au kukitii kile alichosema ukifanye.
JE huko ni kumpenda Mungu kwa NAMNA gani kama hatutaki kumtii yeye.
👉Mungu anatiwazia mema na anasema tutakapomjua ndipo mema ya nchi yatakapotijilia.
Ayubu 22:21
Ndivyo mema yatakavyokujia.
NA hapa ni kwasababu katika hayo yatakufanya kuwa na maarifa zaidi na kumjua Mungu zaidi..kuonhezeka maarifa sana.
Kumbuka kila mafanikio yanahitaji maarifa, na kila unachokihitaji kipo mikononi mwa Mungu, .....lakini cha kushangaza ni kwamba watu wameacha kuyasoma aliyoyasema Mungu mwenye kujua kila kitu lakini wamefuata usomaji wa vitabu vya wanasiasi, wanasaikolojia, wanafalsafa n.k wakiwa na uhitaji wa kupata maarifa ili wafanikiwe.
đź‘ŹSina maana kwamba usomaji wa vitabu hivyo ni vibaya au Labda ni dhambi...hapana Sina maana hiyo !!!
Binafsi hata mimi huwa ninasoma vitabu vingi tu lakini katika hivyo vyote sijaona kilicho bora zaidi kuliko kitabu kimoja tu BIBLIA
Napa nilijua kwanini Mungu anataka niyasome maneno yake.
Mtumishi wa Mungu, naomba ufahamu kuwa shetani hapendi wewe usome Biblia kwasababu anaogopa kwamba Kuna mambo utayajua na utawekwa guru kwa kukujua....lakini kwakutokujua anajua kuwa utakuwa mtumwa wake kila siku.
👉Lazima ujue kuwa Kuna mambo unawekwa guru kwa kuijua kweli tu.
Yohana 8:31-32
[32]tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Lakini Usipojua utaendelea kuangamizwa sana👇
Hosea 4:6
[6]Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
Nakushauri tenga hata wiki moja kila uisome Biblia, tena Anza na virabu rahisi tu...utashangaa mwenyewe kwamba Kuna vitu naanza kuvishangaa, kwasababu utaanza kufurahia kwa kile unachoanza kukielewa na huo utakuwa mwanzo mazuri wa wewe kumuelewa Mungu vizuri.
Mungu akubariki sana nakutakia utekelezaji mwema
KARIBU katika Familia yabutakatifu
KARIBU katika Familia ya maombi
KARIBU katika ukuhani mpya
KARIBU katika unyoofu
Kwa Jina la Yesu.
Mwl / Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni