JINSI YA KUJITENGA NA IMANI
JINSI YA KUJITENGA NA IMANI
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, karibu katika kipindi cha ASUBUHI morning glory ambapo kutakuwa na Maelezo lakini pia sauti ,voice note kwa ufahamu zaidi.
Yuda 1:3-4
[4]Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.
Hpo tunaona Maelezo ya Yuda kuhusu kulionya kanisa juu ya kuishi ndani imani
Kumbuka imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo, (Warumi 10:17 )
Kwahiyo imani yetu kwa Mungu inakuja pale tunapolisikia neno la Mungu la kweli na kukitii.
👉Lakini ukilisikia pasipo kutii maana yake halijengi imani yoyote kwako
👉Au kama umeliasi neno la Mungu yaani hufanyi kama linavyotuagiza maana yake umeikana imani na hiyo ndiyo maana ya kukana imani.
Sasa Yuda aliwaonya kanisa wawe makini kwasababu ya watu wa siri waliojiingiza ndani ya kanisa kama watumishi wa kweli lakini kumbe walikuwa wanafundisha mambo kinyume na Mungu.
Sasa kwanini Yuda alionya watu kuwa makini ??
Ni kwasababu unapoanza KUPOKEA mafundisho ambayo ni kinyume na Mungu maana yake unayaacha Yale ya Mungu yenye kujenga imani na unaanza kuifuta njia nyingine pasipo kujua.
👉Kwasababu imani inaletwa na kuisikia sauti au neno la Mungu mbali na hapo, ukisikiliza kitu kingine mbali na Mungu, maana yake imani Yako inaanza kuwa dhaifu kwa kutokulindwa kwa neno la Mungu na mwisho wa siku unajikuta unatembea kinyume kabisa na Mungu na hapo ndipo unakuwa UMEJITENGA NA IMANI.
👉kujitenga na imani sio lazima usimame na kusema KUANZIA LEO MIMI SIO MKRISTO au Labda KUANZIA LEO MIMI NA IMANI BASI...
Si hivyo...Unaweza kuwa ndani ya ukristo na bado ukajitenga na imani bila kujua, na huku ukitaja jina la Yesu.
👉Kwahiyo Aina ya mafundisho unayoyapokea kutoka kwa watumishi wa Mungu ndiyo yanayokufanya kuacha imani bila kujua au kuendelea kuwa uimara.
👉NA ndiyo maana Yesu akasema " zichunguzeni hizo roho "
👉Lakini nakushauri Leo kwamba isikilize sana Biblia na watumishi Ambao mafundisho yao Yana msingi wa kibiblia zaidi.
NA kwa kufanya hivyo utasimama katika kweli ya Mungu na utakuwa unailinda imani.
👉Usikubali mtu akakulisha kitu ambacho kinaua imani Yako badala ya kukujenga. Kuwasababu unachokisikia na kukiamini huwa ni lazima kikuletee MAJIBU kwenye imani Yako kujengeka au kubomoka.
Neno la Mwisho ..ISHINDANIE IMANI
Mungu akubariki sana
Taifa Teule Ministry
Mwl /Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni