JE MUNGU ANAJIBU MAOMBI GANI ?

 

JE MUNGU ANAJIBU MAOMBI GANI ?

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu

Leo naomba tutazame jambo moja la msingi sana kwa maisha yetu hasa wale ambao huwa wanaomba maombi yao kwa Mungu.

Kila mtu anajua kwamba

👉Tukiomba lolote kwa Mungu tunatendewa

👉Tukiwa na haja ya chochote kile ambacho tunakitamani basi Mungu anatupa

Je ji kweli imani hiyo..?

SI KWELI !🤔

Ni lazima kila mkristo ajue kuwa si kwasababu ni maombi basi Mungu atayasikia na kuyajibu....

WAKO watu wengi ambao aliomba ndani ya Biblia lakini hawakujibiwa majibu yao.

Maombi yanayofika mbele za Mungu huwa yanasifa kuanzia kwa mwombaji, namna ya uombaji na misingi ya uombaji...

Katika ufupi, naomba Kuliweka hili wazi kwako kwamba maombi ambayo yanamfanya Mungu atoe majibu ni maombi sawasawa na MAPENZI YA MUNGU.

KIVIPI ?

👉Kuna mambo ambayo Mungu anahitaji yeye mwenyewe tuwe nayo

👉Kuna niia ambazo Mungu mwenyewe anahitaji sisi tuzipite

👉Kuna viwango ambavyo Mungu anahitaji kila mtu afikie 

👉Kuna maisha ambayo Mungu mwenyewe anataka sisi tuwe nayo 

Na hayo yote yapo ndani ya Biblia.

Soma hapa 👇

1 Yohana 5:14

[14]Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.


Yohana anatupa siri ya maombi yanayosikika mbele za Mungu yaana ni yale ambayo yapo kwenye kusudi lake

Na ndiyo maana mtu anaweza kuwa na mawazo/ hila nyingi ndani ya moyo wake lakini Biblia inasema kuwa SHAURI LA BWANA NDILO LITAKALOSIMAMA


Mithali 19:21

[21]Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; 

Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.

Sasa mapenzi ya Mungu ni yale mambo ambayo Mungu amekwisha ya weka kabisa katika ratiba yake au makusudi yake.

Na unapoomba jambo ambalo lipo nje ya mpango wa Mungu basi juamaombi hayo hayatajibiwa.

👉Lakini unapoyajua mapenzi ya Mungu na ukaomba sawasawa na mapenzi yake kwa jina la YESU basi ni lazima utapokea.


Yohana 15:7

[7]Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

Unaona hapo👆

Katika uchambuzi mzuri wa Biblia hutakuwi kutukia kwenye 

" kuomba mtakalo lolote " Bali unatakiwa kuangalia masharti ya kuomba lolote na kulipokea.

Masharti ni haya

👉Mkikaa ndani yangu

👉Na maneno yangu akakaa ndani yenu

Hapo ndipo mtu anakuwa ana uwezo wa kuomba lolote.

Na Yesu alijua kabisa kwamba mtu akikaa ndani ya Kristo na kisha akaweza KUYASHIKA maneno ya Kristo ( mapenzi yake) na kuyaishi basi ni lazima atakuwa anatembea na kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu kwasababu anakuwa anajua mapenzi ya Mungu ni yapi....

Kwa mfano👇

Waebrania 12:14

[14]Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

Hapo anasema yeye mwenyewe kwamba tutafute kwa bidii kuwa na utakatifu pamoja na amani na watu wote.

Mambo ya Walawi 20:7

[7]Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

1 Petro 1:15

[15]bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;

Unaona katika vifungo vyote hivyo ni kwamba Mungu anataka sisi tuwe watakatifu.

👉Sasa mtu akipiga goti AKAOMBA kwa bidii ROHO YA UTAKATIFU..ni lazima Mungu atampa na kumfundisha kuwa mtakatifu kama Mungu anavyotaka tuwe.

👉Sasa mfano huu nimetoa lengo ujue kuwa MAPENZI YA MUNGU ni sisi kuwa watakatifu hivyo tukiomba utakatifu kwa Mungu ni lazima atatupa kwasababu ndiyo mapenzi au makusudi yake kwetu kwamba tuwe watakatifu.

Na ndiyo maana anasema kuwa yeye huliangalia neno lake ili alitimize....maana yake kwenye neno lake ndimi kunaonyesha mapenzi yake hivyo ukiomba sawasawa na neno lake maana yake umeomba sawasawa na mapenzi yake na UTASIKIKA.

HII ikusaidie kutamani kuyajua mapenzi ya Mungu kwa kusoma neno lake

Tena hii ikusaidie kuwa mkristo mwenye akili anayejua jinsi ya kuomba

Tena ikuponye kupoteza muda na nguvu ya kuomba mambo ambayo si mapenzi yake.....

Mungu akubariki sana


Taifa Teule Ministry

Mwl / Ev Mathayo Sudai

0744474230 / 0628187291 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI