ULIMWOGOPA NANI HATA UKASEMA UONGO ?
ULIMWOGOPA NANI HATA UKASEMA UONGO ?
Bwana Yesu asifiwe ndugu zangu watu wa Taifa Teule la Mungu
Leo ni siku nyingine naomba tuangalie ujumbe huu wa Leo.
Katika ujumbe huu tuangalie jinsi watu wanavyowaabudu watu badala ya Mungu au jinsi watu wanavyoweza kutunza uhusiano wao na watu na faida huku wakiharibu mahusiano Yao na Mungu.
Isaya 57:11
[11]Tena ni nani uliyemwogopa na kumhofu, hata ukasema uongo, wala hukunikumbuka mimi, wala kuweka hayo moyoni? Je! Mimi sikunyamaza tangu zamani, hata huniogopi?
Katika mstari huo unaweza ukaona vizuri na kugundua kuwa Kuna Taifa/ watu/ mtu anayepokea ujumbe kutoka kwa Mungu, kupitia nabii Isaya.
Ukisoma kuanzia mstari wa kwanza unaweza kupata picha kamili
Mungu anasema ni nani uliyemhofu na kumwogopa hata ukasema uongo ?
👉Hapa anatoa kauli nzito kidogo kwa kumshangaa mwanadamu ambaye amekubali kuwapendeza watu fulani na kumwacha Mungu
👉Kuna watu ambao huwa wanaweza kusema uongo mbele za watu viongozi wake bila kujua kwamba anamkosea Mungu.
👉Kuna wengine hufanya jambo la kuwafanya waonekane wema mbele za watu hata kama wako kinyume na Mungu bila hata kujali
👉Kuna watu wengine wanapokuwa wamewakosea watu, huamua kutumia uongo katika kuongea ili pengine wawe salama lakini kumbe wanamkosea Mungu.
Ni lazima ujue kuwa ukimkosea mtu au Ukiwa na uhitaji na kitu kutoka kwa mtu, Basi hutakiwi kutumia uongo au ulaghai wa aina yoyote ili kupata hicho kitu maana Hao ni watu tu bali yuko Mungu ambaye unatakiwa kulinda sana uhusiano wako na yeye uliko wengine wote.
Watu wengine huwa wanapotaka kupata kazi fulani, wanapoona pengine ushindani ni mkubwa..huamua kutoa rushwa ya ngono ili tu wapate kazi hiyo bila kujali kuwa wanamkosea Mungu.
JUA kwamba wa kwanza kumwogopa ni Mungu peke yake na huna haja ya kumhofu mtu yeyote bila kujali umekosea nini au unataka nini.
Isaya 51:12
[12]Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani?
Mtu ambaye ana mwili na atakayekufa hutakiwi kumwogopa..bali mwogope Mungu tu.
👉Mwanadamu hata kama Ana cheo gani, hata kama Ana pesa sana kuliko wewe au Ana chochote kile ..hutakiwi kumwogopa hata ukamkosea Mungu bali yafaa kuwaheshimu wote na siyo kuwaabudu.
Mungu ndiye mfariji wetu
Ndiye msaada wetu
Ndiye kimbilio letu
Ndiye ngome yetu
👉Hivyo tusimwabudu mtu na kumwogopa mtu hata tujavunja mahusiano yetu na Mungu.
👉Ukitembea na haya ninayokwambia watu watakushangaa na kustaajabu juu ya ujasiri wako mbele za watu wote wenye mwili tena utakuwa umetoka kwenye hatari ya kumkosa Mungu
Jambo la msingi ni wewe kujua kuwa UKIMUOGOPA mtu Basi shetani atamtumia huyo mtu kukutoa na hkukuhamisha kwenye mstari wa Mungu.
Moja ya watu watatu ambao shetani mwenyewe anawaogopa ni
MTU ASIYE KUMWOGOPA MTU HATA KUMKOSEA MUNGU
( a man how please men not )
Mungu akubariki sana
Mwl /Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni