HAKUNA CHA KUONGEZA
HAKUNA CHA KUONGEZA Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, Leo nakukaribisha kwenye ujumbe huu wa HAKUNA CHA KUONGEZA. Hebu soma hapa👇👇 Mhubiri 3:14-15 Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye . Hapo tunaona Muhubiri anatuambia vitu kadhaa ambavyo vimebeba maana fulani. Hebu tuvione👇👇 1. KILA ANACHOKIFANYA MUNGU, KINADUMU . Hapa pana siri kubwa ambayo huwa inawafanya watu wa Dunia huu ketuseka bila kujua wafanye nini. 👉Watu wanaweza kuwa na upendo lakini se kama Mungu 👉Watu wanaweza kukupa faraja lakini si kama Mungu 👉Watu wanaweza kukuheshimu lakini si kama afanyavyo Mungu 👉Watu wanaweza kujifanya rafiki zako kwa namna yoyote lakini si kama alivyo Mungu 👉Watu wanaweza kujenga kitu, lakini si kama anavyojenga Mungu 👉Watu wanaweza kukufadhili lakini si kama afanyavyo Mungu, ...