KABLA YA KUMKUBALI MTU ANAYETAKA KUKUOA, SOMA HAPA👇👇

 KABLA YA KUMKUBALI MTU ANAYETAKA KUKUOA, SOMA HAPA👇

Nawakumbusha tena wale mabinti wenye uhitaji wa kuolewa na kuishi katika amani kwenye ndoa zao.

Soma hapa kwa msingi mzuri👇👇

Mwanzo 2:15-17

[15]BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.

[16]BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,

[17]walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

   

Mambo matatu kwa yule atakayetaka kukuoa binti wa LADDIES IN CHRIST lazima awe nayo ni haya

   

 1. Awe na Mungu 

  Mungu alipomuumba Adamu, biblia inasema, alimhweka katika bustani ya edeni

Sasa neno edeni kiebrania lina maana ya Uwepo wa Mungu, pamoja na Mungu, malango ya mbinguni.

 Kwahiyo kabla hujamuuliza swali lingine lolote, jaribu kufuata protocol ya Mungu baada ya kumuumba mtu, akimuweka edeni. Na huyu mtu alipokuwa edeni, alikuwa amekamilika, kwahiyo ili mume wako akamilike ni lazima awe edeni yaani uweponi mwa Mungu, ameokoka vizuri.

   Kwahiyo muulize swali hili,,,UKO HWEPONI. akijibu hapana, usipoteze muda, mwambie akajipange kwanza awe uweponi kama ulivyo wewe, maana huwezi kuwa katika nuru alafu ukatoka nje ya nuru kuungamanishwa na aliye gizani. Huko ni kupotea.


 2. Awe na kazi 

Hili ni jambo la kimaandiko kabisa, na ni protocol ya kimungu kabisa kwamba alipomuumba mwanadamu, akamweka edeni, jambo lililofuata biblia inasema aliwekwa bustani ili AILIME, bustani. Hebu jiulize Mungu anamwambia ailime, ili izae kitu gani angali bustani ilikuwa imejaa matunda?. Kwahiyo utagundua Mungu alifanya jambo la kipekee la kumfanya mwanaume awe na kazi ili ajapo Eva, akute mumewe ana kazi, japo hili ni jambo la pili la muhimu sana, kwamba kijana kabla ya kuoa lazima awe na kazi. Yaweza kuwa si kuajiriwa lakini awe angalau mtu wa mizunguko huku na kule kutafuta kipato. Sio kijana anaishi kwa mjomba wake, sijui kwa dada, au bibi, hana hata dalili za kumiliki japo nyumba ya chumba kimoja japo kupanga, au yupo tu hata mwenyewe pesa ya vocha inamshinda, alafu kwa matamaa yake ya ngono anakuja kukwambia anataka kukuoa. Na wewe kwasababu unahitaji na shauku kubwa ya kuolewa unakubali tu. Binti yangu nakupa pole kwa huo msiba hiyo ni mauti. Kwahiyo muulize,,,,UNAKAZI?, AU UNAJISHUGHULISHA? 

. Na hakikisha kazi yake unaijua,

Sio mtu anakwambia mara oooh siunajua tena, tupotupo tuuu, tunapambana mara, vyuma vimebana,,,aa hapana lazima ujue anajishughulisha na nini kupata kipato.

   

 3. Awe na uwezo wa kukutunza

Ukisoma hapo vizuri utaona tena biblia inasema, kwamba Adamu, alipowekwa edeni, ili ailime pia na AITUNZE.

   Kwahiyo ili kijana awe amekamilika lazima pia aweze kukutunza, mwingine anaweza kuwa na hivi vyote viwili lakini hataki kukuhudumia. Anaweza kuwa amepata pesa, ukashangaa tu siku hiyo amekuja kavaa suti mpya, alafu nyumbani hakuna chakula, au vitoto vinatembea peku, au mama huna hata vitenge. Jua hiyo ni hatari.

   Jambo hili ndilo leo unaona kwenye ndoa nyingi, baba anarudi anasema ameshiba ameshakula hotelini, na nyumbani hawajala au mama kahangaika wamekula japo dagaa, ila baba hali anadai ameshakula, kama mama tambua tu hapo kuna kitu hakipo sawa, huyo mume hajui kutunza.

  Au unakuta baba anatangulia kwenda kanisani anamwacha mama maana hataki waongozane, kwasababu yeye kapendeza kuliko mkewe, ni hatari sana.

   Yani ukiona mume anataka kupendeza kuliko wewe mkewe anza kupiga goti kumuomba Mungu. Ni jambo la ajabu sana, we hata hushangai anataka kupendeza sana kuliko wewe ili iweje?. Kwahiyo lazima huyu kijana anayetaka kukuoa aonyeshe kukujali wewe kuliko anavyojijali yeye, ndiyo ishara kwamba anaweza kukutunza.

  Kwwhiyo kabla ya kumkubalia muulize ,,,VIPI, UNAWEZA KUNITUNZA?. 


Binti wa LADDIES IN CHRIST, Ni tumaini langu kuwa umeelewa maswali muhimu ya kuyapatia majibu kabla hujamkubali mtu.

 Jambo hili ni la msingi sana na litakusaidia sana kuepukana na vijana wa ajabu wanaotamani kulala na wewe tu na si ndoa au upendo.


0628187291/ 0744474230

      Ev. Mathayo Sudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI