NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE
NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE
Bwana Yesu asifiwe Watu wa Mungu, naomba kueleza kidogo kuhusu wa mstari huu👇👇
Waebrania 13:4
Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Hapo kuna mambo machache ya muhimu katika mistari huu ambayo tunaweza kuiachambua👇👇
1. NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE
Sasa lazima tufahamu kwanini Mungu anazungumza na sisi tuliookoka kwamba, ndoa na iheshimiwe na watu wote?
Baada ya Adamu na hawa kuumbwa, Mungu aliendelea kuijaza dunia na ku andaa Watu wake kwa kupitia jambo hili yaani NDOA.
Soma hapa👇👇
Mwanzo 2:23-24
[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
[24]Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Unaona jambo hili la ndoa halijawekewa heshima na maelekezo Jana au juzi, Ni jambo lililopewa uzito na Mungu mwenyewe toka EDENI kabla ya anguko.
Ndoa ndiyo njia pekee ya kimaandiko iliyotumiwa na Mungu kuweka mahusiano na wanadamu wake, kwa kuijaza dunia hadi Leo hii. Ni jambo la msingi sana👇 mbele za Mungu na ndiyo maana akasema IHESHIMIWE NA WATU WOTE.
2. MALAZI YAWE SAFI
Hapa Mungu anazungumza na wale ambao watakuwa tayari katika ndoa, kwamba kila mmoja, awe mwaminifu kwa mwenzake.
Kwa tafsri nzuri ya kiingereza Soma hapa👇👇
Hebrews 13:4 (NLT)
Give honor to marriage, and remain faithful to one another in marriage. God will surely judge people who are immoral and those who commit adultery.
Au Soma hapa👇👇
Hebrews 13:4 (KJV)
Marriage is honourable in all, and the bed undefiled: but whoremongers and adulterers God will judge.
Hapo tunaweza kuona kuwa Biblia inatukumbusha, tunapokuwa katika ndoa zetu, basi kila mmoja awe mwaminifu kwa mwenzake, yaani kitanda chenu kisichafulize na uchafu wa kitanda kingine.
Hili ni lazima tuleelewe vizuri na ndiyo maana tunasema Watu wawe makini kabla ya kuoa au kuolewa.
Usije ukashindwa kuwa mwaminifu kwa mwenza wako, ukaitoa heshima ya ndoa ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.
3.WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU ATAWAHUKUMIA ADHABU
Hapo nyuma ametuambia tuwe waaminifu kwa wenza wetu, na hapa anatoa moja wapo ya madhara ambayo Mungu atawapa Watu ambao watashindwa kuwa waaminifu. Wazinzi
Utakaposhindwa kuwa mwaminifu na kutoka një ya ndoa utakuwa umeondoa heshima ya ndoa, umeyachafua malazi na umekuwa MZINZI.
Lakini Mungu atakuhukumia adhabu.
JE! Ni adhabu gani?
Soma hapa👇👇
Ufunuo wa Yohana 21:8
[8]Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na WAZINZI, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Mimi ni ndugu yako niliye mdogo kuliko wote
Na Mungu akubariki sana. 🙏🙏
Maoni
Chapisha Maoni