HAKUNA CHA KUONGEZA

 HAKUNA CHA KUONGEZA

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu,

Leo nakukaribisha kwenye ujumbe huu wa HAKUNA CHA KUONGEZA.


Hebu soma hapa👇👇

Mhubiri 3:14-15

Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.

Hapo tunaona Muhubiri anatuambia vitu kadhaa ambavyo vimebeba maana fulani. Hebu tuvione👇👇


1. KILA ANACHOKIFANYA MUNGU, KINADUMU.

Hapa pana siri kubwa ambayo huwa inawafanya watu wa Dunia huu ketuseka bila kujua wafanye nini.

   đź‘‰Watu wanaweza kuwa na upendo lakini se kama Mungu

   đź‘‰Watu wanaweza kukupa faraja lakini si kama Mungu 

   đź‘‰Watu wanaweza kukuheshimu lakini si kama afanyavyo Mungu

   đź‘‰Watu wanaweza kujifanya rafiki zako kwa namna yoyote lakini si kama alivyo Mungu

   đź‘‰Watu wanaweza kujenga kitu, lakini si kama anavyojenga Mungu

   đź‘‰Watu wanaweza kukufadhili lakini si kama afanyavyo Mungu,

     Pamoja na kazi nyingi sana ambazo wanadamu huzifanya kwa akili zao wenyewe, sote huzifanya lakini si kama afanyavyo Mungu.

   Swali ni👉Si kama Mungu kivipi?

Ni kwamba Mungu hufanya kwa mkono hodari na kazi yake huwa inadumu, yaani si ya muda mfupi kama ilivyo kazi ya mwanadamu.  

🙏Mungu akikufadhili, basi fadhili zake ni za milele


 Soma hapa👇

Zaburi 106:1

Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.


🙏Mungu akikupenda, basi pendo lake imara kweli kweli

   Soma hapa👇

1 Yohana 2:5

Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.

🙏Mungu akikubariki, basi baraka yake inakutajirisha kabisa


Soma hapa👇

Mithali 10:22

Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo.

✋✋✋ Hivyo ni lazima leo ufahamu kwamba, wanadamu huchoka kukusaidia ila Mungu hachoki, yaani Mungu akiisha kuangalia tu basi utamuona katika uzuri wote unaodumu milele na milele.

Lakini hatari huwa ikaanza pale ambapo mtu anatumia nguvu na akiri zake, na baadae alichokipata kinaposhindwa kudumu anarudi kulalamika, mara ooh mbona kila siku mimi tu, mara oh mbona sifanikiwi kumbe hajui kuwa anatumia akili zake tu wala si Mungu na huku anahitaji kubarikiwa baraka za kudumu.

Sifa ya Mungu ni kwamba anapokubariki, anakewekea na ulinzi kwa vile alivyokupa kwahiyo shetani hawezi kuharibu,.

Lakini usipomweka Mungu mbele basi jua utakachokipata, hakina ulinzi wowote, hivyo kitavamiwa na kwasababu hiyo hakitodumu milele. Na hii ndiyo sababu Mungu anafanya vitu vinavyodumu.

Hata vitu alivyoviumba Mungu, mpaka leo bado vipo kwasababu alipovifanya aleweka na namna ya kuviendesha kwa nguvu yake mwenyewe.


2.CHA MUNGU HAKIONGEZEWI WALA HAKIPUNGUZIWI KITU.

Shetani hajawahi kuumba kitu chochote duniani maana hata yeye aliumbwa na Mungu, alikuwa malaika aina ya kerubi.

  Kwa maana hiyo hajaumba kitu pia hawezi kuumba.

Kwahiyo kile alichokiumba Mungu ndicho kile kile hakijawahi kuingezwa na mtu au kitu chochote walabhakijawahi kupunguzwa.

Unaweza kuuliza mbona maadili, utakatifu na upendo vimepungua na wakati anaumba ulimwengu hali haikuwa hivi?

✋Upendo, maadili na utakatifu havikuumbwa na wala haviwezi kuumbwa, kwasababu hizi ni hali zinazotokana na mtu kuweza au kushindwa kukaa na Mungu.

  Kwa mfano, Mungu hakuumba dhambi, ila dhambi ni ile hali ya mtu kutokutii maagizo ya Mungu tu basi.

Kwahiyo hizo ni hali tu zinazokuja kulingana na jinsi mtu anavyoishi na Mungu.

Lakini Muhubiri anatuambia kuwa kazi ya Mungu haiongezwi wala haipunguzwi.

Kumbe ni lazima utambue kuwa Mungu akifanya kazi ya kufunga, huwa hapawezi kufunguliwa na mtu mtanga afungue yeye na akifungua vivyo hivyo hakuna anayeweza kugusa kazi ya Mungu na kuamua kufunga isipokuwa Mungu mwenyewe.


Soma hapa👇

Luka 21:15

kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.

Mungu akikupa kitu kamili, basi tambua hakuna mtu wa aina yoyote anayeweza kukipunguza kwa namna yoyote kwasabab kazi anayoifanya Mungu huwa haipunguzwi wala kuongezwa na mwanadamu.

Hebu hii ikupe shauku ya kuhitaji kukaa na Mungu vizuri, ili atakapokubariki basi wasiwepo wenye kuweza kuchezea baraka yako. Lakini mtu akiamua kuzitafuta baraka kwa watu, wenye moyo wa nyama, wanaochoka, wanaolala na kusinzia basi ni lazima atambue kwamba wapo watu ambao wanaweza kupunguza, kukiharibu au kukiangamiza kwa laana, uchawi, na njia nyingine

Hata leo epuka kuwategemea watu badala ya Mungu kwasababu vitu vyako vitapunguzwa na kuisha bila kujua.


Soma hapa👇

Yeremia 17:5

BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

Mtegemee Mungu na mruhusu aifanye kazi yake kwako, hakika haitapunguzwa na mtu wala kuongezea mabalaa na mikosi kwasababu asili ya kile kinachofanywa na mkono wa Mungu, ni hii KIMEKAMILIKA.


3. ILI WATU WAMCHE MUNGU

Unajua watu wengi hawajui kwanini Mungu hufanya kazi katika ukamilifu, na kwanini anachokifanya anakiweka kidumu. 

Lakini leo naomba kukwambia kwa uzuri kabisa kwa Mungu hufanya hivyo kwasababu👇

ANAKUPENDA SANA WEWE NA HATAKI UABUDU KITU KINGINE. 

Unaweza kujiuliza anakupenda sana kivipi? 


Soma hapa👇

Yohana 3:16

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Huu👆 ni mstari ambao umewakaa watu wengi sana kichwani lakini hawaelewi siri yake ni nini. 👇

Ni hivi👉 Baada ya Adamu kuasi na dunia nzima kuwa upotevuni, ilikuwa na maana kuwa wote tulikuwa tumepotea, tulikuwa tunaelekea mautini tu na tukahesabiwa watu wa jehanamu tu kwa uasi uliokuwepo kwasababu hakukua na mtakatifu wa kumpendeza Mungu na wote tulikuwa tayari kwa hukumu. 

Lakini kwa upendo wa ajabu wa Mungu aliyekuwa anatakiwa kutuhukumu, akamtuma mwanae wa pekee, narudia mwanae wa PEKEE Yesu, jambo lililopelekea sisi kufutiwa hukumu na kuwa wasio na hatia lakini si hivyo tu, pia akatufanya kuwa watoto wake✋ huo ni upendo wa ajabu sana. 

Yaani kuifuta hukumu yako na kukufanya uwe mtoto wake. Halleluyaaaa

 Na ndiyo maana Yohana alilifikiria sana hilo akasema👇


1 Yohana 3:1

Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo......


HIVYO BASI Mungu huzifanya kazi zake zote kwa namna tuliyoiona kwasababu ANAKUPENDA SANA

Na pia ANAHITAJI UMUABUDU YEYE TU.

Kama Mungu angekuwa anafanya kazi zake kwa udhaifu, basi watu wasingetosheka ingebidi watafute msaada na pengine lakini yeye anafanya kwa ukamilifu kabisa ili tusiwe na uhetaji wa kitu yaani tusipungukiwe. Na ndiyo maana Daudi aliliona hilo akasema hivi👇


Zaburi 23:1

BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.

Kwahiyo kwa kuwa na mahusiano mazuri na Mungu basi utakiri kama alichokiri Daudi. Leo hii watu wanashindwa kusema neno hilo la kutokupungukiwa kwasababu wanatumia sana akili zetu, tunatumia sana waganga na watu wa dunia hii jambo linalopelekea kukosa vitu vyenye ukamilifu.


Iakini wamesahau kuwa Mungu anawivu sana na yeye alisema👇👇

Kutoka 20:3

[3]Usiwe na miungu mingine ila mimi.

   Na alisema hivyo kwasababu yeye anakila kitu katika ukamilifu, na ukiwa na Mungu tu bila michanganyo ya miungu basi, haupungukiwi.


Mungu akubariki sana

Taifa Teule Ministry

Mwl/Ev. Mathayo Sudai

0744474230 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI