MKE MWEMA NI NANI,,,,?
MKE MWEMA NI NANI,,,,?
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, nina wasalimu kaika jina la Yesu Kristo aliye Bwana na mokozi wa maisha yetu.
Leo natamani tujifunze jambo moja fupi sana kuhusu mwanamke mema.
Imekuwa ni kawaida kwa wanawake wengi, mamia yao, au wanapokutana wawili au watatu na wakaanza kuzungumzia kuhusu watu walionao kwenye mahusiano ya kimapenzi, ambao kwa namna moja ama nyingine wanajiandaa kuingia nao kwenye maisha ya ndoa pamoja nao.
Mara nyingi sana, inapozungumzwa jambo hili, huanza kwa kuulizana swali hili...wewe boyfriend wako anafanya biashara gani au kazi gani?
Kimaandiko na kimantiki, jambo hili si vibaya hata kidogo kama litaishia na swali hilo tu. Na ni vizuri sana kwa mwanaume kuwa na kazi au kipato kwa lengo la usalama wa familia kama nilivyokwisha kufundisha kwenye masomo mengine yaliyopita, bofya hapa==https://elimuyabiblia.blogspot.com/2022/11/kabla-ya-kumkubali-mtu-anayetaka-kukuoa.html
Kwa usalama wa maisha yako kama binti wa kikristo, tusome hapa chini
Mithali 31:10.
“Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? maana kima chake chapita kima cha marijani.”
Kwa kupitia mstari huu mmoja tu unagundua kumbe kuna tofauti kati ya mwanamke, na mwanamke mwelevu au mwema.
Ameanza kwa kusema mke mwema ni nani awezaye kumwona, akiwa na maana kuwa mwanamke mwema, mwenye namna hii, kwanza si watu wote huweza kuwa na sifa zake na ndiyo maana pia si kila mwanamume anaweza kumuona maana anasifa za tofauti na wanawake wengine.
· Wakati mabinti wengine au wanawake wengine wanakimbilia kwa waganga kutaka kupata mume, yeye huwa hafanyi hivyo
· Wakati wanawake wengine wanahangaika na kujichoresha kwa wanaume wenye pesa na maarufu, yeye huwa hana wala hata haitaji kujipitisha kwa wanaume hao.
· Wakati wanawake wengine
· Mitindo ya mavazi ambayo huwa wanawake wengi wanahangaikia kuivaa, yeye huwa hana mpango nazo
· Kitu kinachakasirisha wanawake wengine na hata kutoa lugha chafu, yeye kina mfanya kufikiri
· Kile kinachosemwa na wanawake wengi duniani, yeye huwa hakisemi
· Mawazo yake ni matakatifu na ni salama kwa jamii
· Mwanamke huyu si wa kawaida kama walivyo wengine, maana hubadilisha kila mazingira yanayowatesa wengi, yeye huyashughulikia na kupata suluhu
· Dunia hufikiri kuwa mwanamke wa asili hii hayupo ni kwasababu wanaume wengi hawana macho ya kumuona mke wa namna hii.
· Mke huyu si mke wa kushinda kuongea na simu na mpenzi wake kuanzia asubuh hadi jioni.
· Si binti wa kuchati na simu mpaka usiku wa manane, kwa madai anaongea na mpenzi wake
· Huyu ni mke anayejiheshimu sana.
Na sifa nyingine nyingi za mke mwema.
Leo hii unaweza kusikia wanaume wengi kila sehemu wanasema kuwa, HAKUNA MKE WA PEKE YAKO, wakiwa na maana kuwa ukioa mke, basi tambua UMEOA WEWE ILA WANAMTUMIA WENGI. lakini hawajui tu kuwa yupo mwanamke ambaye, ukiwa naye ndani huna wazo la kumwekea mlinzi wa kumlinda ili kutunza mapenzi yenu na huyu si mwingine bali ni mke mwema.
PIA BIBLIA IKASEMA.
‘’kima chake chapita kima cha marijani’’
KIMA wakati mwingine huitwa BEI
MARIJANI ni aina ya madini yenye langi iliyo katikati ya waridi/pinki na nyekundu iliyokolea na kwa lugha ya kiingereza madini haya huitwa ruby, ambayo kimsingi yana thamani kubwa sana.
Sasa Biblia inasema kuwa mwanamke mwema ni yule ambaye bei yake ni zaidi ya bei ya ruby, ikiwa na maana kuwa mke mwema ni yule ambaye
· Hamkubali mtu eti kwasababu anamiliki makampuni
· Hamkubali mtu eti kwasababu ana kazi kubwa inayompa kipato cha juu sana
· Hamkubali mwanaume kwasababu ya umaarufu wake
· Hamkubali mwanaume kwasababu ya utajiri aliokuwa nao
Bali mwanamke huyu humkubali mtu kulingana na maelekezo maalumu yaliyotoka mbinguni na kibali ambacho amepata ndani ya moyo kwa kuangalia sifa tatu muhimu, kama nilivyoeleza kwenye somo lililopita la kabla ya kumkubali mtu angalia mambo 3.
Hii ikiwa na maana kuwa mke mwema bei yake ni kubwa kuliko fedha na si fedha ambayo inaweza kumnunua mke huyu bali ni maelekezo maalumu kutoka mbinguni na upendo wadhati kutoka kwa mwanaume.
Hivyo basi mabintio ndani ya Kristo, usiishi kama mwanamke wa dunia hii asiyelitunza agano lake na Mungu.
Ishi kama mke mwema ambaye sifa yake kuu ni hii AMETOKA KWA MUNGU.
Ukiwa na sifa hii inatakiwa ujue kuwa mwanaume mpumbavu hatokuwa na uwezo wa kukutaka ili akuchezee, bali jua atakayekuwa na uwezo wa kukutaka basi anajicho la kuona thamani uliyonayo tofauti na wake wengine.
Pia si gharama kuwa mke mwema, maana ndivyo alivyo huyu mke mwema yani hizo ndio sifa zake za kila siku.
Mimi ni Mathayo Sudai niliye mdogo kuliko wote, na Mungu akubariki.
Maoni
Chapisha Maoni