USIENDELEE KUKAA, AMKA TEMBEA MBELE

 


USIENDELEE KUKAA, AMKA TEMBEA MBELE.

Bwana asifiwe wana wa Mungu, nawakaribisha katika siku ya Leo katika kujifunza ...

Leo natamani kusema na wewe juu ya Hali ambayo inawaua wengi pasipo wao wenyewe kujua na wamebaki kuishi katika Masha ambayo hayako vizuri huku wao wakiwa ni mashahidi wa ubovu wa maisha Yao....

jambo hili huwa linaanzia pale mtu anapoanguka, dhambini au mambo Yale kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu....

watu wengine wakianguka dhambini huwa wanakata tamaa moja kwa moja,

👉Kama walikuwa wanahuduma, wanaiacha kabisa

👉Kama walikuwa wanaenda kanisani, ghafla waaacha

👉Kama walikuwa wanaomba basi utakuta hawapmbi Tena kwasababu wanajisikia wakavu kabisa..

👉Kama walikuwa na ratiba za ibada nyumbani, au ratiba za mambo ya kimungu kama semina, mikesha, kufunga,n.k basi wanajikuta wanaacha...

SASA, Hapa ni lazima ujue sababu ya wao kushindwa kweda mbele ni MASHTAKA KUTOKA KWA SHETANI..., kwasababu SHETANI ndiye mshitaki na si Mungu...


1 Petro 5:8

[8]Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.


Ufunuo wa Yohana 12:10

[10]Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

SHETANI huwa anaanza kumwambia mtu kwamba

👉 hafai mbele za Mungu, au

👉Mungu Hana Furaha na wewe, 

👉Maombi yako hayasikiki, 

👉Toba yake haijasikika kwa Mungu,  n.k

Wakati mwingine utakuta mtu huyu ameifanya dhambi hiyo au ameanguka na dhambi hiyo mara kadhaa,  na hapo SHETANI atamwambia maneno ambaye muhisika atayasikia kama mawazo yake, na yeye mwenyewe utakuta inafika hatua anajiona kama mnafiki mbele za Mungu na anajiona mzito kwenye mambo ya Mungu na anabaki kuishi hivyo tu.

LAKINI 

Leo natamani ujue kitu Cha msingi Sana kuhusu Mungu alivyo katika maisha yako...

KWANZA . .. Tambua kwamba Mungu siyo mtu/Mwanadamu ambaye huwa anaweza kukuweka moyoni lakini Mungu ni Mwenye rehema na unapoomba yeye huwa anasikia.

kwahiyo USIENDELEE KUKAA chini hata kama Kuna dhambi uliifanya kwasababu, gharama za kukaa hapo ni kubwa Sana... tunapooishi kwenye maisha ya wokovu basi ni lazima utambue kwamba ni maisha ya Vita hivyo SHETANI anapokupiga na akakufanya kutenda dhambi haimaanishi kwamba inatakiwa kukata tamaa Bali simama na uendelee kusonga mbele.... 


 hebu Soma hapa👇

1 Yohana 2:1

[1]Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki...

Mungu hataki tutende dhambi, Neno hili halimaanishi ukae kwenye anguko Bali kama ukitenda dhambi bas rudi utubu na Kisha ujue Yesu yupo ambaye ndiye mwombezi...

lakini pia tambua jambo hili hapa👇


Mithali 24:16

[16]Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.


AMKA TENA NDUGU, MUNGU ANAKUITA .......

Usikae hapo ulipo kwenye udhaifu na makwazo bali yakupasa uendelee... kumbuka gharama ya kukaa hapo chini ni kubwa Sana...  hata Mungu anakutaka uamke...


Isaya 52:1

Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.


Mungu akubariki Sana


Min. Mathayo Sudai






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI