BUSARA ITAKULINDA...



                  BUSARA ITAKULINDA....
Bwana Yesu asifiwe Wana wa Mungu, ni siku nyingine, karibu tujifunze jambo la msingi linalohusu BUSARA...

Mithali 22:3
Mwenye busara huyaona mabaya na  kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.

👉unapokuwa na BUSARA maana yake unakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.... 
👉unakuwa na uwezo wa kuamua lililojema kwenye maisha yako bila kujali linaumiza kiasi gani katika maisha ya kawaida

Biblia inaweka wazi kwamba Watu wanaweza kuona jambo fulani baya ambalo limetokea au linataka kutokea...
Sasa, ukiwa na BUSARA maana yake ni lazima ujitenge na hayo mabaya kwa njia ya kujificha mbali nayo...

Biblia inaposema kujificha... maana yake kufanya Jambo au kusimama katika mahali ambapo baya hili halikupati...
👉unapoona Kuna watu wanafanya mabaya yenye madhara, na wewe ukaamua kutembea mbali nao ili madhara hayo yasikupate hapo unakuwa umejificha
👉unapoona Kuna madhara ya uovu yanakuja kuwapata watu, halafu ukaamua kukaa mbali na uovu hapo umejificha
👉pia hata katika maisha ya mwilini tu, unaweza kuliona tatizo fulani linakuja kwako na madhara, wewe unapoamua kujitenga na tatizo Hilo maana yake umejificha
👉unapoacha kugombana na mtu ili kuepusha madhara, hapo unakuwa umejificha kwa BUSARA...

Busara inamfanya MTU kusimama katika Hali ya usalama mbali na Yale ambayo yanaweza kumdhur... na ndiyo maana Biblia inasema hivi kuhusu burasa...👇

Mithali 2:11
Busara itakulinda; 
Ufahamu utakuhifadhi.

unapokuwa na BUSARA
👏unajitenga na magomvi
👏unajitenga na malumbano
👏unajitenga na uovu
👏unaitenga na maamuzi yanayoumiza 
👏unajitenga na utendaji kwa hasira... kwasababu busara inakupa kujificha mbali na mabaya...

hata Yesu Mwana wa Mungu alipoyaona madhara ya wanaotaka kumpinga kabla ya wakati wake alijificha...

Yohana 8:59
Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.

lakini Biblia inasema WAJINGA HUENDELEA MBELE WAKAUMIA

yaani si lazima kila ubaya unatakiwa kupambana nao, Kuna mengine hayana maana kwako yapishe maana ukiyafuata kushindana nayo basi wewe ndiye utakayeumia au dhulika...
👉si kila mtu anayekutukana,unatakiwa kumshambulia hebu tumia busara na ujifiche
👉si kila aliyeinua mikono kukuua unatakiwa kumwinulia na wewe Bali wengine wapishe na ujifiche katika mikono ya Mungu 
👉si kila aliyekusema vibaya unatakiwa kumjibu na kumshambulia Bali nyamaza tu maana hiyo ni busara..
👉ukiwa mtu wa kuyafuata mabaya nasi kuyapisha kwa BUSARA basi utajikuta unaumia Sana kwenye maisha.

Mungu akubariki Sana

Minister Sudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WANAWAKE 21 KATIKA BIBLIA NA MAHUDHUI YAO

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA