NANI YUKO NYUMA YAKO


NANI YUKO NYUMA YAKO

by Min. Mathayo Sudai

Bwana asifiwe...
Tumshukuru Mungu kwasababu tupo salama...

Tujifunze kitu  hapa 👇

Kuna njia nyingi sana ambazo watu huzitumia pale wanapokuwa katika utafutaji mbalimbali...
👉Kuna wanaowategemea watu
👉Kuna watu wanategemea mali zao
👉Kuna watu wanategemea waganga na wachawi kila mtu na namna yake...
👉Kuna wengine wanamtegemea Mungu
👉na Kuna wengine wanategemea akili zao tu

hizo zote ni nguvu ambazo zipo nyuma ya watu ambao wanatafuta au kuchakalika katika maisha Yao...

lakini Soma hapa👇

Mithali 23:4
[4]Usijitaabishe ili kupata utajiri;
Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.

Biblia inaposema usijitaabishe, haina maana kwamba usifanye kazi, au usitafute kazi.... lakini kujitaabisha panapozungumzwa hapo ni kule mtu kujiwekea nguvu kutoka kwa watu au kutumia nguvu zake tu ili kufanikisha Jambo...

lazima ujue kwamba kutenda jambo kwa namna hiyo hakuleti mafanikio... kwasababu, ... kama mkristo unatambua kwamba tunapokuwa tunashindana hatushindani na mtu Bali adui yetu yupo katika ulimwengu wa roho...

yaani Ile nguvu inayokuzuia si ya mtu Bali ipo katika Roho (Waefeso 6:12)

Sasa kwa mantiki hiyo basi unatakiwa kuwa na nguvu kubwa nyuma yako ili kila utakachokifanya kifanikiwe... na nguvu  hiyo si nyingine Bali MUNGU MWENYEZI....

👉Unapofanya biashara hakikisha nyuma yako kuna nguvu ya Mungu inayokupa kushinda
👉Unapofanya huduma Basi Usitumie ujuzi na nguvu zako tu Bali awepo Mungu...
👉Hata unaposoma n.k Basi hakikisha nyuma yako kuna nguvu ya Mungu inayokusaidia...

nguvu ya Mungu ndiye kuu kuliko zote alizonazo adui..

1 Yohana 4:4
[4]Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.

kwahiyo tunapomtegemea Mungu maana yake tunamtegemea aliye mkuu kuliko adui yetu....

na katika msisitizo huo Biblia inasema USIZITEGEMEE AKILI ZAKO.

Hapa ni lazima ujue kuwa akili ya mtu huwa Ina mpaka wake katika utendaji.... yaani Kuna majibu fulani utayapata kwa akili ya kawaida tu na Kuna mengine Huwezi kuyaweza kwa akili zako...

lakini hata kama Kuna majibu fulani katika akili yako basi jifunze kujua kwamba Mungu ndiye aliyeweka maarifa hayo ndani ya mtu...

mahali ambapo unashindwa kutenda basi..
👉usianze kumwabudu mtu ukidhani anaweza kukusaidia.                                        👉usimtegemee Shetani na usinyenyekee kwake maana kitendo hicho ni kuuza nafsi yako kwake

👉USIZITEGEMEE AKILI zako

Bali hapo unatakiwa kumtazama Bwana, maana yeye ndiye anayetupenda na hapendi tuteseke...

Mungu akubariki Sana

Taifa Teule Ministry

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI