WEWE NI RAIA WA NCHI GANI?


      WEWE NI RAIA WA NCHI GANI?

Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu... karibuni katika tafakari nyingine ya leo ndani ya TAIFA TEULE MINISTRY, na leo tutajiuliza kwamba sisi ni watu au wenyeji wa nchi gani....

ni lazima ufahamu kuwa katika jicho la Mungu au kibiblia ni kwamba kuna nchi mbili tu ambazo ni 

✋Nchi ya nuru yaani mbinguni na 
✋nchi ya giza...

na hizi zote zinawenyeji au raia wake ambao wanahusika na katika watu wote ulimwenguni kote, basi wanaingia katika makundi haya mawaili aua katika nchi hizi mbili,.. 

kama ilivyo mwilini, kwamba kila mtu unayemjua ni lazima awe na nchi yake pengine mkenya, mtanzania, mrundi, mrwanda, mmarekani n.k yaani kila mtu ana nchi wala hutasikia mtu akisema kuwa yeye hana nchi au Taifa. na hivyo ndivyo ilivyo katika ulimwengu wa roho, kila mtu ana nchi yake na hakuna mtu asiye na nchi katika zile nchi mbili yaani giza na nuru...

kumbuka Biblia hupenda kutumia neno ufalme, Taifa, miliki n.k kuonyesha au kuitaja NCHI

kitu gani kinachomfanya kuitwa mkenya, au mtanzania au mmarekani?, ni desturi na tamaduni ambazo mtu huyo anazo,,, kila nchi huwa ina utamaduni ambao wananchi wake wanakuwa nao....

Wafilipi 3:20 
Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo.

kumbe unapokuwa umempokea Kristo Yesu na kutembea kwenye wokovu unakuwa na urithi katika ufalme wa Mungu, mbinguni na hii ni kwasababu unakuwa unaonyesha au unaishi kwa desturi ya mbinguni
na usipokuwa na desturi ya mbinguni maana yake unakuwa na desturi za nchi nyingine na si nyingine ila ni gizani

WAEFESO 5:5
 Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, (ndiye mwabudu sanamu), aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu

kumbe kuishi katika dhambi yaani kuufuatisha mwili ni desturi ya gizani wala si nuruni na ndiyo maana aishiye kwa jinsi hiyo, hana nafasi katika ufalme wa nuru na si raia wa nchi ya mbinguni...

kila ufalme huwa ni lazima uwe na mfalme, hivyo Yesu ni mfalme wa nuruni na shetani ndiye mfalme wa giza...

WAFILIPI 2:1-2
Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;

Huyu mfalme wa anga ndiye shetani na ndiye anayetenda kazi kwa watu wake hata sasa yaani wana wa kuasi, wale wasiomtii Mungu YEHOVA...

Hii inatusaidia kujua kwamba mtu asipokuwa na utii au kumuheshimu Mungu, basi tunajua si yeye bali yupo chini ya mamlaka ya mfalme wa nchi yao ambaye yeye ndiye anayemwongoza, na ndiyo maana wengi wanaishia kuingia kanisani tu ila si kumtii Mungu, na hilo linasababisha wao kuendelea kuwa watumwa wa shetani kwasababu hawajamtii Mungu....

Shetani hana shida wala hamuogopi mtu anayeingia kanisani, bali anamuogopa mtu ambaye hukaa uweponi mwa Mungu, huzungumza na kumtii Mungu... na anachokifanya ni kuwapotezea watu wengi Muda kwa kujivunia makanisa yao tu na huku mioyoni mwao wako mbali sana na Mungu.... na ndiyo maana leo hii utasikia watu wanagombana kisa madhehebu huyu anasema dhehebu lake ndilo bora na huyu naye anavutia kwake, lakini hao wote hawajui kuwa wanapotezewa muda na mfalme wa giza na mwisho wake wanatii sana taratibu za madhehu yao kuliko sheria za Mungu...

Na kumtoa mtu kwenye ufalme mmmoja kwenda mwingine inahitajika sadaka fulani na ndiyo maana Yesu alimwaga damu yake msalabani ndipo akatutoa katika ufalme wa giza na akatuweka kwenye ufalme wake....

WAKOLOSAI 1:13-14
Naye alituokoa kutoka kwa nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa;  ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.

Sadaka hii ni sadaka ya milele ambayo Yesu aliitoa kwwjili ya watu wote na kwasasa ili utoke gizani na kwenda nuruni ni rahisi sana yaani KUAMINI, na baada ya hapo KUKIRI KWA KINYWA CHAKO

WARUMI 10:9-10
 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu....

ukiishi kwa taratibu za gizani basi jua JEHANAMU ndiyo urithi wako, na ukiishi kwa taratibu za mbinguni basi ufamle wa Mungu ndiyo urithi wako, yaani una nafasi katika ufalme wa Mungu....

JE WEWE NI RAIA WA NCHI GANI....? Tamani kuwa katika ufalme wa Mungu kwa kumpokea Yesu leo...

MUNGU AKUBARIKI SANA

Taifa Teule Ministry
Min. Mathayo Sudai



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI