WAAMBIE MABINTI WATAZAME VYEMA



   WAAMBIE MABINTI WATAZAME VYEMA

Asifiwe Yesu wana wa Mungu.....

Leo natamani ujifunze jambo moja la msingi sana kwenye maisha yako....

NI HIVIπŸ‘‡

Mithali 21:2
Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo. 

kila mtu huwa ana namna yake ya kufikiri anapohitaji kufanya jambo fulani, na vile anavyofikiri mtu ni njia ya kipekee ambayo inampeleka mtu katika kufanya uamuzi wa jambo husika.

hii ina maana kuwa vile afanyavyo mtu ni matokeo ya vile alivyokuwa amewaza au kufikiri kwenye jambo hilo... na ndiyo maana Biblia ikasema " Awazavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo "

Sasa mtu anapowaza jambo katika namna fulani, basi huwaza kwasababu ya namna ambavyo alilitazama jambo hilo na wengine hulitazama jambo baada ya kuwa wamewaza katika namna fulani....

Sasa nini bora, kufikiri baada ya kutazama au kutazama baada ya kufikiri ?

Maamuzi ambayo mtu atayachukuwa kwa " kufikiri baada ya kuona " yanaweza kuwa na tofauti kubwa sana na maamuzi anayofanya mtu kwa " kuona baada ya kufikiri "


MFANO KATIKA MAHUSIANO

Kuna mabinti ambao huwa wanawaza aina ya mume au aina ya ndoa wanayotaka kuiishi kabla hata ya kukutana na mwanaume wa kuwaoa, na kuna wanaowaza hayo yote baada ya kuwa kuna mtu amewafuata kuonyesha nia ya kuoa....

Maana yake kuna aliyefikiri kabla/kwanza na kuna aliyeona kabla/kwanza... nadhani unaanza kunielewa

πŸ‘sasa kama ni hivyo maana yake kuna uwezekano wa mtu kutazama ndivyosivyo kwasababu aliwaza ndivyosivyo pia ni rahisi mtu kuwaza vibaya kwasababu aliona tofauti....
πŸ‘Kama wewe ni binti unayehitaji kutembea katika usahihi basi ni lazima uwe unawaza au kufikiri kabla hujafanya jambo lolote.... hapa nini maana kuwa ni vizuri ukawaza kwamba
πŸ’₯ndoa yako iweje
πŸ’₯Mume wako aweje
πŸ’₯aina gani ya familia uwe nayo
πŸ’₯aina gani ya maisha unayahitaji kwako
πŸ’₯Aina gani ya mahusiano unayahitaji....

Ninaposema kwamba MUME AWEJE, sina maana ya urefu, ufupi, mweusi au mweupe bali ninamaanisha sifa za ndani za huyo mwanaume.... unaweza kufikiri na kusema....

πŸ‘‰Nahitaji mume mwenye uwezo wa kunifundisha yaani awe anajua kuliko mimi
πŸ‘‰Nahitaji mwanaume ambaye anauwezo wa kuijali familia
πŸ‘‰Nahitaji mwanaume ambaye ataweza kuwa na mimi kwenye nayakati zote
πŸ‘‰Nahitaji kuwa na mwanaume mwenye upendo wa kweli ambaye hata akipata kitu hatanisaliti
πŸ‘‰Nahitaji mwanaume mwenye Mungu.....
πŸ‘‰Pia unaweza kuwaza na kusema nahitaji mwanaume yeyote tu, hii nayo inawezekana....

Sasa unapokuwa umewaza kuhusu ndoa au familia yako au mume na ukawa katika kuomba basi mtu yeyote atakapokuja itakuwa ni rahisi sana kujua kwamba anafaa au hafai.... na hautaruhusu kila mwanaume kukugusa na kukupotezea thamani....

πŸ‘Lakini ukimuona ndipo ukaanza kufikiria basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kumkubali bila kujua kwamba ni sahihi au la kwasababu amekuja ukiwa unahitaji mume sana, na hivyo uwezo wako kufikiria utakuwa ni kumkubali zaidi kuliko kumkataa.... utaanza kuwaza kwamba nikimkataa itakuwaje na muda unaenda, nikimkataa itakuwaje kama ndiye aliyekusudiwa na Mungu n.k na hiyo ni kwaababu ulishindwa kufikiria kwanza na badala yake ulianza kufikiria baada ya kumwona mume....

Usipofikiria basi hata ukija kumwona inawezekana kabisa kwamba ukaona vibaya na ukafanya maamuzi mabaya... lakini ukiwa tayari umeshafikiria na kuomba basi ni rahisi sana kugundua kwamba ni yeye au la... na ndiyo maana Bibli imesema kwamba...

Mithali 21:2
Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo.

Sasa kumbe Mungu hupima MOYO, na sisi tunajua kwamba moyoni mwa mtu ndipo mahali ambapo mawazo ya mtu yapo/hutoka,

πŸ’₯Unapoona na ukafanya maamuzi, hiyo ndiyo njia uliyoichagua lakini usahihi au ubovu wa hayo maamuzi hupimwa moyoni, yaani katika mawazo yako uliyokuwa umeyawaza mwanzoni

πŸ‘‰Ulimpenda mume kwasabbau ya wazo la kupata fedha kwake, magari, nyumba au kwasababu ya namna alivyo mbele za Mungu ?
πŸ‘‰Ulimpenda na kumkubali huyo mwanaume kwasababu au kwa lengo gani... hicho ndicho anachokiangalia au kukipima Mungu katika njia ya mtu... YAANI MOTIVE YAKO NI NINI....

kumbe ili kuwa na njia ambayo ni sahihi lazima tuwe tumeweka msingi katika moyo ambako ndiko hupimwa na Mungu..

ukijua mapenzi ya Mungu basi fikiria sawasawa na mapenzi ya Mungu, ukifanya hivyo maana yake hata Mungu anapopima moyo wako anakuta umewaza sawasawa na mapenzi yake na hiyo inakupa kupata kibali mbele zake yaani kujibisa ....

1 YOHANA 5:14-15
Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tunapoomba chochote, tunajua kwamba tumetimiziwa zile haja tulizomwomba.

Tambua kwamba... "ukifikiria vizuri, basi utaona vizuri, na ukiona vizuri basi utachagua au kufanya maamuzi sahihi"

UKIFIKIRI SAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU, BASI UTALITAZAMA JAMBO KAMA MUNGU ATAZAMAVYO NA MAAMUZI YAKO YATAKUWA SAHIHI SAWASAWA NA MUNGU APENDAVYO

Mungu akubariki binti wa Yesu

Laddies In Christ
Min. Mathayo Sudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI