MLIKUWA MKIPIGA MBIO VIZURI NI NANI ALIYEWAZUIA ......??

MLIKUWA MKIPIGA MBIO VIZURI NI NANI ALIYEWAZUIA ......??

Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu....

leo ni siku nyingine, karibu tujifunze na kujikumbusha jambo la msingi kwaajili ya maendeleo ya imani zetu...

WAGALATIA 5:7-9                                                                                                                                          Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 8 Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi. 9 Chachu kidogo huchachua donge zima

sasa ukiangalia vizuri huo mstari utagundua kwamba Paulo alizungumza na Wagalatia katika namna hiyo kwasababu aliona kuna jambo ambalo limefanyika na watu wamelifanya kuwa ndiyo utaratibu, angali si uharisia.

wagalatia walipokuwa wamempokea Yesu Kristo kwa kinywa cha Mtume Paulo, walikuwa wakitembea katika uharisia wa injili katika imani...lakini baada ya muda kupita, Paulo alikuja na kuwakuta wanatembea katika namna nyingine tofauti na vile walivyopokea....ndipo akawauliza mbona mlikuwa mnaenda vizuri kipindi cha nyuma je ni NANI aliyewazuia msiitii kweli?...

hakusema je ni nini....bali je ni nani...

NINI Maana yake kitu, lakini NANI maana yake kuna mtu.

hii inatusaidia kufahamu kwamba kurudi nyuma kwa wagalatia hawa ilikuwa ni kwasabbau kulikuwa na nguvu ya ziada kutoka kwa adui ambaye alikuwa amewafanya warudi nyuma na kuacha kutembea kwa imani na hata kurudi nyuma kwenye sheria yaani walinaswa kwenye yale waliyokuwa wakiyatenda nyuma kabla ya kumpokea Yesu....

neno hilo tunaliona tena kwenye kitabu cha mwanzo, wakati Mungu alipokuwa akiongea na Adamu baada ya kuwa ameanguka......

MWANZO 3:9-11                                                                                                                   9 BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 10 Akasema, Nilisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. 11Akasema, Ni NANI aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?

UNAONA HAPO...hata Mungu, alijua kwamba anguko la Adamu si kwasababu ya kitu bali kuna mtu/kiumbe fulani chenye uhai kilichohusika....na ndiyo maana akasema NI NANI.

sasa hapo tunaona kwamba tunapokuwa tumeokoka kunakuwa kuna nguvu ya ziada kutoka kwa adui yaani shetani kwa lengo la kuturudisha nyuma na kutunasa kwenye maisha au utaratibu ule wa zamani ambao ninyume na mapenzi ya Mungu...ni lazima kama mkristo ufahamu kwamba unapokuwa umetangaza vita na adui shetani kwa kuokoka maana yake yeye hulenga kukuvuta kule nyuma....lakini ashukuriwe Mungu atupaye kushinda tena zaidi ya kushinda...

kuna watu ambao wanatembea kwenye wokovu, huku wakiwa na maizigo yao ya zamani ambayo ni kinyume na Mungu...jambo hilo linapelekea safari ya wokovu, au tendo la kupiga mbio kuivuata taji liwe gumu kwao kwasababu ya hiyo mizigo....na ndiyo maana hata katika maisha ya kawaida kwa wale wanaofanya mchezo wa riadha/kukimbia..huwa ni lazima wasibebe mizigo ili isije ikawamaliza nguvu na kushindwa kupiga mbio vizuri....jambo hilo hata kwenye wokovu ni sawa na ndiyo maana Biblia ikasema hivi👇

WAEBRANIA 12:1                                                                                                                         Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa subira katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu

👉unapokuwa kwenye wokovu na huku unazini kwa siri jua kabisa kuwa unajichosha na unajichelewesha                                                                                                                                         đź‘‰unapokuwa unamwabudu Mungu huku unachuki na kuwasengenya watu kwa mabaya basi unajichelewesha                                                                                                                                        👉yaani kuchanganya wokovu na dhambi ni kujikwamisha mwenyewe na kupoteza muda

usikubali kuwa na michanganyo bali muheshimu Mungu na usonge mbele....

SASA, Paulo naye alijua kwamba kuna watu au nguvu fulani iliyowafanya wagalatia waanze kutembea nje na imani huku wakijiita wakristo hivyohivyo....

lakini pia akasema....Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi. 9 Chachu kidogo huchachua donge zima

yaani yule aliyewashawishi au kuwaongoza hivyo si Mungu...kwasababu Mungu hawezi kukutoa kwenye njia sahihi ya imani na kukuweka na ndiyo maana Paulo akawa na uhakika kabisa, kwamba kwa mwenendo huo, Mungu hajahusika bali ni adui...

lakini akasema unavyoendelea kutembea kwenye wokovu huku umebeba chachu/uovu wa kale basi itafika kipindi utachachuka kabisa...yaani uovu utakutawala kabisa....

mara nyingi moja ya njia za mtu kufa kiroho, ni kutembea na uovu bila kuushughulikia kiasi kwamba uovu unazidi kukua na hata mwisho wake kukuangamiza..na kwa hapa unatakiwa kuwa mtu ambaye unapoona uovu ndani yako tu basi sogea mbele za Mungu, kiri hiyo dhambi na umwambie Mungu akusamehe na kukusaidia...UTAKUWA SALAMA....


MUNGU AKUBARIKI SANA


Taifa Teule Ministry                                        
    Min. Mathayo Sudai
    0744474230/071473229


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI