WEWE NI RAIA WA NCHI GANI?
WEWE NI RAIA WA NCHI GANI? Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu... karibuni katika tafakari nyingine ya leo ndani ya TAIFA TEULE MINISTRY, na leo tutajiuliza kwamba sisi ni watu au wenyeji wa nchi gani.... ni lazima ufahamu kuwa katika jicho la Mungu au kibiblia ni kwamba kuna nchi mbili tu ambazo ni ✋Nchi ya nuru yaani mbinguni na ✋nchi ya giza... na hizi zote zinawenyeji au raia wake ambao wanahusika na katika watu wote ulimwenguni kote, basi wanaingia katika makundi haya mawaili aua katika nchi hizi mbili,.. kama ilivyo mwilini, kwamba kila mtu unayemjua ni lazima awe na nchi yake pengine mkenya, mtanzania, mrundi, mrwanda, mmarekani n.k yaani kila mtu ana nchi wala hutasikia mtu akisema kuwa yeye hana nchi au Taifa. na hivyo ndivyo ilivyo katika ulimwengu wa roho, kila mtu ana nchi yake na hakuna mtu asiye na nchi katika zile nchi mbili yaani giza na nuru... kumbuka Biblia hupenda kutumia neno ufalme, Taifa, miliki n.k kuonyesha au kuitaja NCHI kit...