USIYAKUBALI MASHTAKA YA SHETANI
USIYAKUBALI MASHTAKA YA SHETANI
Na. Min
Mathayo Sudai
Bwana Yesu asifiwe watu wa MUNGU, leo ni siku nyingine
nakukaribisha kwenye ujumbe mzuri ambao utakusaidia kusonga mbele kwa jina la
Yesu…..
Ni mara nyingi katika dunia hii, watu wengi wanamjua Yesu au
wanaokoka baada ya kuwa wameishi kwenye dhambi kwa muda mrefu….
Sasa wanapookoka huteswa na hali zao za nyuma za yale maisha
ya dhambi kwasabbau ndani ya mawazo/ akili zao huanza kujiona kana kwamba
wanamaovu mengi, hawastahili kusimama mbele za Mungu na jambo hili hupelekea
kuwa na wasawasi juu ya hata zile toba ambazo walifazifanya. Huanza kuwa na
mashaka na hata kudhania kuwa maombi yao hayasikiki kabisa mbele za Mungu …na
madhara ya jambo hilo ni kwamba WANASHINDWA KUSONGA MBELE….
Lakini ashukuriwe Mungu aliyetupa neno lake kwa kinywa cha
mtume Paulo kusema hivi…
WARUMI 8:1-2
1 Kwa
hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu, wale
ambao hawaenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho. 2 Kwa sababu sheria
ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na
mauti.
Unaonma hapo, kumbe unapokuwa ndani ya Kristo Yesu wewe
huhusiki tena na mashtaka ya yale maovu ambayo uliyafanya….na si hivyo tu hata
unapokuwa umeokoka na ukajikwaa yaani ukatenda dhambi, basi ni lazima ujue
kwamba ukitubu tu Mungu anakusamehe na anayasahau kabisa makosa yako yote…..na
hapo kinachofuata ni kwamba shetani ataanza kukukumbusha zile dhambi
ulizozifanya, atakukumbusha kwamba kuna siku ulizini na mtu, atakukumbusha
kwamba kuna siku ulilewa pombe na ukawatukana watu, atakukumbusha kwamba wewe
uliiba, au ulidanganya na mengine mengi tu…..
Na kuna wengine hata wanapokuwa wanaomba au wanasoma neno la
Mungu na kulitafakari, ghafla hushangaa wanaanza kukumbuka dhambi zao jambo linalowafanya
washindwe kusonga mbele kwasabbau ya kujiona mchafu….
Hata shetani anajua kwamba ukiwa unaomba au unasoma neno la
Mungu, anajua kabisa kwamba unafanya jambo zuri na la msingi sana ambalo
linaleta hasara kwa ufalme wake, sasa anachokifanya ni kukuletea kumbukumbu za
mambo uliyowahi kuyafanya…utaona wewe mwenyewe unaanza kujidharau na kusema
kwamba “mimi siwezi kumwimbia Mungu maana
ni mchafu” , au “mimi sifai mbele za
Mungu kwa yale niliyoyafanya “ au ”ivi dhambi zangu zilisamehewa kweli”…..
Na wakati mwingi shetani atawatumia watu ambao waliwahi
kukuona ukifanya dhmabi na wataongea maneno ya kukudharau sana….
Jambo hilo linakufanya unashindwa kusonga mbele kabisa kwa
kujiona hufai….
Lakini leo natamani ujue kuwa tunapookako historia zetu mbaya
zote hufutwa
Isaya 43:25 “Mimi,
naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako, kwa ajili yangu mwenyewe, wala
sizikumbuki dhambi zako tena.
Kama mkristo ni lazima ujue kuwa ndani mwetu hutunzwa taarifa
ya kila kitu ambacho mtu anakiwaza, ambacho uliwahi kukisema, kukifanya,
kukitafakari na pale mtu anapokufa Mungu anaziweka wazi kazi zote ambazo
uliziendea huyo mtu…lakini katika ulimwengu huu na ulimwengu wa roho, kuna
nguvu moja tu ambayo inaweza kufuta historia mbaya yote ambayo ulishawahi
kuiweka, na hiyo nguvu inaitwa DAMU YA YESU……Haleluyaaaa…
Kumbe tunapotubu dhambi maana yake tunakombolewa kwa kutolewa
kwanye maisha ya dhambi….
WAKOLOSAI 1:13-14
13
Naye alituokoa kutoka kwa nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika
ufalme wa Mwana wake mpendwa; 14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani,
msamaha wa dhambi.
Sasa kama tunasamehewa dhambi maana yake tunakuwa wapya kwa
kuingizwa kwenye ufalme wa Mungu na tunaanza maisha mapya ndani ya Kristo….
2 WAKORINTHO 5:17 Hata
imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita,
tazama! Yamekuwa mapya.
Sasa kuokoka kunatufanya sisi kuwa na wakili mwaminifu yaani
Yesu Kristo ambaye yeye ndiye anayetutetea pale hukumu inapotaka kusimama kwetu…yaani
ni hivi,……unapotenda dhambi maana yake lazima upate mshahara wako yaani mauti
lakini unapochukua hatua ya kutubu na kuoshwa kwa damu ya Yesu ni kwamba
inapotakiwa kusimama ile hukumu YESU mwenyewe anasimama kwenye hiyo kesi na
kusema kwamba “MIMI NILISHAKUFA TAYARI
KWAAJILI YA MAKOSA YA HUYU MWANANGU “ …..na hiyi ndiyo maana Biblia inasema
tunapokuwa katika Kristo basi hauna kukumu kwetu kwasababu yupo anayesimama
kututetea na kuizuia hukumu…..
WAKOLOSA2:14
akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake,
iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
KWAHIYO mtu wa Mungu ni lazima ulijue hilo ili shetani
asipate nafasi ya kukuzuia kusonga mbele kwa kujiona kuwa ni mchafu, hufai n.k…
Na unapokuwa unajihusisha na maombi au kusoma neno au jambo
lolote lile na ghafla mshtaki wetu yaani shetani akakukumbusha mambo ya nyuma
ambayo pengine yanakuumiza basi hapohapo anza kusema maneno ya ukiri na
kutanganza kama haya …NIMEKOMBOLEWA KWA
DAMU YA YESU, HATA SASA MIMI NIMWANA WA MUNGU NILIYEZALIWA SI KWA DAMU AU KWA
NYAMA BALI NI KWA ROHO, KAMA ILIVYOANDIKWA KWAMBA NINAPOOKOKA YA KALE YAMEPITA
SASA YAMEKUWA MAPYA NA MIMI NAKATAA MASHTAKA YA KIPEPO KWA JINA LA YESU, KAMA
ILIVYOANDIKWA KATIKA WARUMI 8 YA KWAMBA HAKUNA HUKUMU JUU YA WOTE WALIO NDANI
YA KRISTO YESU, NAMI LEO NASIMAMA KINYUME NA MASHTAKA AMBAYO SHETANI ANAYATUMIA
KUNIRUDISHA NYUMA, NINAYAPINGA KWA DAMU YA YESU, NINAYAKATAA KWA JINA LA YESU…..MIMI
NI WAJUU SIKU ZOTE MAANA NIMEKETISHWA PAMOJA NA KRISTO KATIKA MKONO WA KUUME WA
MUNGU…IMEANDIKWA KWAMBA BWANA ATAYASAHAU MAKOSA NA DHAMBI ZANGU NAMI KWA IMANI,
NINAYAKATAA MASHTAKA YOTE YA MWOVU SHETANI NA NINAKIRI UZIMA, AFYA, AMANI, NA
USHINDI KWA JINA LA YESU…..
ukiwa ni mtu wa kusema maneno kama hayo katika uombaji wako basi shetani
atajua wewe si mjinga bali unafahamu kuwa wewe ni nani…na nikuhakikishie kwamba
utaendelea kusonga mbele bila kurudi nyuma kwasababu ya hayo mashtaka ya adui
Mungu akubariki sana
Taifa Teule Ministry Min. Mathayo Sudai
0744474230
Maoni
Chapisha Maoni