JE WAFILIPI 2:3 INA MAANA GANI
Bwana Yesu asifiwe Wana na Binti za MUNGU.
leo Ni siku nyingine tutaiangalia ujumbe ndani ya kitabu Cha Wafilipi 2:3
Wafilipi 2:3-5
[3]Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.
hapo Kuna mambo kadhaa ambayo hatupaswi kuyashika pale ambapo tutakuwa tunaendenda katika Utendaji kazi wetu..
Biblia imesema tusifanye Neno LOLOTE kwa
1: KUSHINDANA
Hapa Biblia inalenga kutufanya tusiwe watu wa kufanya Mambo kujionyesha kana kwamba sisi Ni Bora kuliko watu wengine katika hali ya UBINAFSI..usifanye Jambo kwa kupambana na mwenzako huku ukimuonea wivu...
...wivu ndiyo hufanya watu kufanya jambo kwa mashindano mioyoni mwao huku wakitamani wao ndo waonekane na kusifiwa mbele ya kanisa kuliko wenzao....
👉ukiwa na tabia ya KUSHINDANA kwa UBINAFSI ndani ya Ufalme wa MUNGU Basi jua haikubaliki kabisa ndani ya Ufalme wa MUNGU
👉Mungu anataka watu tushirikiane na tuwe nania moja ya kulifikia lengo ambalo Mungu anataka wote tufikie
👉usiposhindana na mtu Basi utamsaidia.....
👉Hata katika maisha ya wokovu unaweza kukuta watu wanashindana kwenye huduma huku lengo la Ni kujitukuza na kuonekana wao kuwa Ni Bora mbele za watu...
👉Mungu ametupa agizo sisi wote ndani ya wokovu na ili sisi tulikamilishe yafaa tushikane na siyo KUSHINDANA kwa ubaya..na huku kila mtu akitaka kuonekena Bora kuliko wenzake.....yafaa kumtukuza Mungu na si kujitukuza wenyewe...
👉 Kama kweli wote mnafanya lile analolihitaji Mungu Basi haina haja ya KUSHINDANA Bali kushirikiana Ni Bora Sana
👉mpaka kufikia mnashindana kiwivu na ubaya Ni ishara pekee kwamba hamfanyi mapenzi ya Mungu Bali mnafanya ya kwenu na kila mtu anatafuta kutukuzwa mwenyewe.....
LAKINI LEO TAMBUA KWAMBA KAMA UNAFANYA MAPENZI YA MUNGU BASI USISHINDANE NA ANAYEFANYA MAPENZI YA MUNGU PIA BALI MSHIKAMANE NA KUWEZESHANA kila mtu akimthamini mwenzake......
2: MAJIVUNO
Pia hili Ni Jambo ambalo hatutakiwi kuwa nalo kwenye maisha yetu ...
👉MAJIVUNO yanasababisha MTU kuacha kumtukuza Mungu na kunyenyekea badala yake anajiinua yeye na kujisifu ndani take kuwa yeye Ni Bora zaidi.....
👉Kuna watu hujiona kuwa bila wao ndani ya kanisa, Basi HAKUNA litakalofanyika...yaani wanajiweka katika nafasi kana kwamba wao ndio kila kitu...
👉ukiona uko hivyo maana Yake ndani yako una MAJIVUNO...yaani kujiinua...
👉Sasa ukiona una Hali hiyo juq kabisa kwamba huna unyenyekevu na anguko lako lipo karibu, kwasababu ya hicho kiburi
Mithali 16:18
Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
hata shetani mwenyewe alikuwa na kiburi na kujiona kana yeye ndio kila kitu na yeye ndiye anayestahili kuabudiwa....lakini baada ya kujiona hivyo Heshima mbele za Mungu ikapotea na ndipo anguko lake likafuata...
hivyo Kama mkristo na mtu unayempenda na kumuheshimu Mungu Basi usiwe mtu wa MAJIVUNO kwa kinywa chako, au kwa moyo wako...maana haimpendezi Mungu
👉Ukiwa na MAJIVUNO utaona wenzako hawafai isipokuwa wewe tu ndio mzuri na unayefaa
👉Jambo hilo huua huduma na karama za wengi kwasababu Mungu huacha kuwatumia kwasababu ya MAJIVUNO Yao pale wanapotumika mbele za Mungu ......
👉👉Baada ya Mambo hayo Biblia inamaliza mstari wa tatu kwa kusema tuwe na Nia Kama alivyokuwa nayo Yesu....
Ni ipi hiyo....??
NI Ile ya kuwahesabu wengine kuwa bora kuliko sisi...
Yesu ni Mungu lakini alituona sisi Ni Bora akaamua kuja kufa msalabani kwaajili yakutukomboa ....
aliacha Heshima yake, kuabudiwa kwake na kuheahimiwa Kama mfalme Mbinguni badala yake akaamua kujishusha , kutemewa mate, kupigwa, nankusurubishwa hata kufa kifo Cha aibu...lakini yote Ni kwasababu ALITUONA SISI NI BORA ....
Wafilipi 2:4-8
[5]Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
[6]ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
[7]bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
[8]tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
MUNGU AKUBARIKI SANA
Mwl/Ev. Mathayo Sudai
0744474230/0714732009
Maoni
Chapisha Maoni