JE UNAPENDEZWA NA MATENDO YA MUNGU
JE UNAPENDEZWA NA MATENDO YA MUNGU
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu
Leo ni siku nyingine, karibu tutazame jinsi matendo ya Mungu yanavyomfunua mtu wake.
Zaburi 111:2
[2]Matendo ya BWANA ni makuu,
Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.
Anasema kuwa matendo ya Mungu ni makuu, 🙁
NA jambo kama hilo ni dhahiri kwamba kila mtu analifahamu vizuri
👉Kila MKRISTO, ukimuuliza habari za Mungu na matendo yake, anaweza akaanza kukusimulia kuanzia Mungu kuwatoa wana wa Israeli Misri mpaka walipoingia katika nchi ya ahadi.
👉Atakwambia kuhusu habari za nyoka wa shaba
👉Atakwambia habari za chakula cha mana n.k
NA kimsingi mambo hayo watu huyajua toka wanavyokuwa watoto wadogo kwenye shule za watoto ( Sunday school )
Lakini hayo yote hayafunui upendo wa mtu kwa Mungu, wala hayaonyeshi mahusiano ya mtu na Mungu.
Biblia inasema WANAOPENDEZWA na matendo makuu ya Mungu, huwa na muda wa kuyatafakari, kuyafikiria sana Yale ambayo Mungu huyafanya na zaidi ya yote katika kuyafikiria hayo huishia katika kumtukuza Mungu.
NA Mungu hutukumbusha watu wake juu ya Yale aliyoyafanya akiwa na lengo kwamba, matendo yake yawe kama sehemu ya fikra zetu na sehemu ya maisha yetu ili sifa na utukufu virudi kwake milele
👉Tena ni lazima watu wa Mungu wajue kuwa hakuna mtu anayeweza kumsifu na kumtukuza, na kumheshimu Mungu kama fikra yake haina ukuu wa Mungu.
👉Sababu ya kwanini watu Wengi wamejiingiza kwenye mambo ya Dunia na kile wanachokiita ujana na udada ni ukosefu wa HOFU YA MUNGU, lakini hii HOFU YA Mungu inakuja ndani ya mtu pale anapokuwa na wema, fadhili,upendo na matendo makuu ya Mungu ndani ya Moyo wake.
Kutoka 20:20
[20]Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi.
Utisho wa Mungu aunaopatikana kwenye kile alichokifanya lengo lake ni kumfanya mtu asitende dhambi.
Lakini swali linakuja hapo👇
KWANINI WATU WANATENDA DHAMBI ANGALI MUNGU AMEFANYA MENGI KWA WATU
Jibu ji Kwamba watu hawa huwa hawayatafakari matendo makuu ya Mungu bali wanajua tu habari za Mungu kama hadithi za kawaida.
.na ndiyo maana Mungu anatutaka kwamba maneno yake yasitoke vinywani mwetu tena tuyatafakari
Yoshua 1:8
[8]Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Hakuna mtu anayeweza Kumpenda Mungu na asiwe na HOFU YA Mungu
👉Tena hilo lipo kwa wale wanaopendezwa na matendo makuu ya Mungu
.je wewe unapendezwa na matendo makuu ya Mungu ???
Je una HOFU YA Mungu ??
JE unampenda Mungu unavyojiona wewe ??
JE wewe huyatafakari matendo ya Mungu
Hebu chukua wakati kidogo tafakari kuanzia kule alikokutoa Mungu mpaka hapo ulipo kisha angalia namna inavyoishi ( unavyomlipa Mungu ) halafu chukua hatua
KUMBUKA Mungu humtoa mtu sehemu moja na kwenda nyingine kwa utukufu wake tu,
Hivyo yatafakari matendo ya Mungu kwako na Yale yote uliyosikia akiyafanya kisha HOFU YA Mungu iwe pamoja na wewe.
Zaburi 4:4
[4]Mwe na hofu wala msitende dhambi,
Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
KUMBUKA
MUNGU NI MUNGU WALA HUKUNA ANAYEWEZA KUMBADILISHA
Mungu akubariki sana🙏
Taifa Teule Ministry
Mwl /Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni