USIPENDE KUWA MFU



 USIPENDE KUWA MFU

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, karibuni katika kujifunza ujumbe huu wenye hitaji la kukuimarisha katika pendo la Yesu na imani tuliyoachiwa kwa uweza wa Roho mtakatifu. 

  Mfu ni mtu au mnyama asiyekuwa na uhai. 

Kitu au mtu anapokuwa katika hali ya kufa huwa anakuwa na sifa zifuatazo

👉Haoni chochote

👉Hasikii neno lolote 

👉Hatambui kitu

👉Haongei kitu

👉Hawezi kufanya kazi yoyote ile. 

Sasa Paulo aliwaambia waefeso kuwa hata wao walikuwa na hali hiyo. 

Soma hapa👇

Waefeso 2:1-3

[1]Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;

[2]ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;

[3]ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.

Alitoa sababu ya mtu kuwa mfu, na unaposoma vizuri unagundua kuwa anaongea na watu waliyo hai, lakini anasema hapo mwanzo walikuwa wamekufa.

  🤔Kumbe kufa si lazima uwe umekufa kimwili na kuzikwa,

🤔Kumbe mtu anaweza kuwa anatembea angali amekufa

🤔Kumbe unaweza kuishi na mtu ambaye amekufa na bado anatembea.

Lakini anatoa maana ya kufa kiroho au kuwa mbali na kusudi la Mungu, kwamba ni walikuwa wafu kwa makosa na dhambi zao ambazo walikuwa wanazifanya zamani kwa kuifuta njia au kawaida ya ulimwengu huu.

Mtu wa Mungu natamani ufahamu neno hili kwamba 👉mtu anayeishi kwa namna ambayo watu wa ulimwengu wanaishi kinyume na Mungu basi huyo ni mfu

👉Mtu ambaye anafanya mambo ambayo wa ulimwengu wanayafanya naye huyo ni mfu hata kama anaingia kanisani kila siku.

👉Mtu ambaye moyoni mwake haoni shida kuutunza udunia na mihemko ya kipepo huyo naye ni mfu kiroho.

Hawa wenye nanma hiyo ni watu ambao Biblia inawataja kuwa ni wafu kwasababu

  Ya namna maisha yao yalivyo yanadhihirisha kwamba hawa si mali ya Kristo, yaani wanafuatisha desturi ya watu wa dunia na wala si tabia ya Roho mtakatifu. 

Ni lazima tujue kuwa hai kunakozungumzwa ni kuwa chini ya mamlaka na kuongozwa na sheria ya Roho mtakatifu, 

Hebu soma hapa👇

Warumi 8:9

[9]Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.

👏Sasa Paulo anasema kufa ni kuifuata kawaida ya ulimwengu, 

  Tena hapa anasema kama Roho wa Mungu anakaa ndani yako basi kamwe huwezi kuufuata mwili. 

😯Na anasema mtu asipokuwr na Roho wa Mungu huyo si mali ya Krsto. 

🤔Na kama huyo si mali ya Kristo tafsiri yake huyo mtu ni mfu kwasababu ya tamaa za mwili na njia za ulimwengu anazoziendea. 

Siku hizi kuna kituko huwa kinatokea kwa wale wanaojiita wakristo, 

 Utakuta kila mtu akiwa anajitambulisha, anataja jina na anamalizia kwa kusema NIMEOKOKA NAMPENDA YESU. 

Lakini utakuta anafuatisha kawaida ya ulimwengu, wala hamtii Roho mtakatifu na haongozwi na Roho wa Mungu. 

Kivipi? 

Ni hivi👇

👉Ivi utasemaje umeokoka wakati hata kwenye simu yako tu umejaza nyimbo za kidunia na unaziimba kabisa. 

👉Utasemaje una Roho mtakatifu angali, wewe kuongea maneno mabaya kwako siyo shida

👉Utasemaje umeokoka na unampenda Yesu angali wewe unashabikia mambo ya kidunia, wewe kuingia disko huoni shida, kucheza nyimbo za kidunia huoni shida, 

Ukiona unafanya vitu kama hivi na bado unadai umeokoka na kanisani unaingia kwa ujasiri na huoni shida kuyafanya hayo na unayafanya tu, basi nakupa pole kwa pesa unazoziita sadaka ambazo huwa unazitoa kanisani kwenu kwasababu unapoteza ni bora ungefanya mambo mengine. 

Na siku hizi kuna watumishi ambao wanaihitaji pesa yako na ndiyo maana hawaisemi kweli wanaendelea kukuongoza tu bila kujua wanapotea na kuwapoteza wanaowaongoza, yaani ni wale ambao Biblia inawaita vipofu. 

Utakuta wanahubiri, eti hata kama una dhambi kiasi gani, ukitoa sadaka tu unafanikiwa,..... 

Ndugu huo ni uhuni wa kiroho kwa wanaojiita wakiroho. 

Hebu soma hapa👇

Tito 1:15-16

[15]Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.

[16]Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.

Vitu vyote vinafaa kwa walio safi na anasema hakuna kilicho safi kwa walio najisi. 

 Najisi ni nani? 


Marko 7:21-23

[21]Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

[22]wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

[23]Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.

Na ndiyo maana kwa namna ya dunia ambayo unaiendea inaendelea kukufanya kuwa na moyo unaotoa vitu vinavyokunajisi wewe bila kujua. 

 Na hivyo vitu vyako si safi. 

Na anasema wanakiri kuwa wao ni wakristo na wanamjua Mungu lakini kwa matendo yao wanamkana tena hawafai kwa tendo jema. 

🙂Unajua, ukiwa na Roho mtakatifu, ni lazima matunda yake yaonekane kwake. 

Matunda ya Roho ni nini? 

Matunda ya Roho ni asili au tabia za Roho mtakatifu zinazoonekana kwa mtu. 

Kwamfano 

👉Roho anasifa ya upole

  Kwahiyo mwenye Roho mtakatifu ni lazima tabia hii ionekane kwake

👉Roho ni mtakatifu na anachukia dhambi

  Hivyo aliye na Roho mtakatifu, lazima awe na sifa hiyo. 

Na hii ndiyo maana ya matunda ya roho, na ukiona huna matunda ya Roho bazi lazima uanze kujua kuwa hauna Roho mtakatifu. 

Na kama huna Roho mtakatifu basi wewe si milki ya Kristo :Warumi 8:9, Warumi 7:14-15

Na kama wewe si wa kristo basi umekufa. 

Tabia au matunda ya Roho ambayo kila mwenye Roho mtakatifu ni lazima yaonekane kwake ni haya👇


Wagalatia 5:22-26

[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

[23]upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

[24]Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

[25]Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

[26]Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.

Sasa 

👉wawezaje kuwa na Roho mtakatifu anayependa manyimbo ya duniani yasiyo na utukufu, 

👉Wawezaje kuwa na Roho mtakatifu anayekufanya uwe na mihemko ya ujanani, mihemko ya uzinzi, ulevi, matusi, masengenyo n.k

Huyo si Roho mtakatifu ni roho ya shetani. 

Jichunguze rafiki , acha kupoteza muda, tupo kwenye kipindi kibovu ambacho Mungu anahitaji walio tayari siyo wanohitaji kuvutwavutwa. 

Na hiki ni kipindi ambacho Yesu baada ya kuingea mengi akasema maneno haya👇

Ufunuo wa Yohana 22:11-12

[11]Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

[12]Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

Ukiona hutaki kuisikiliza sauti ya Mungu, basi Yesu anasema endelea na uzinzi wako, endelea na uchafu wako, endelea kuufuata mwili na mihemko ya kipepo

Lakini jua anakuja kukulipa sawa na ulivyo, na hapo ndipo utakapojua kuwa Mungu hadhihakiwi 

Wagalatia 6:7

[7]Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

Injili ya namna hii watu huamka na kusema MBONA UNATUHUKUMU, 

 Na husema hivo kwasababu ya aina ya wale wanaowafundisha wamewazoesha kufarijiwa hata kama wanatenda dhambi, 

Na Biblia inawaita watumishi hao kuwa mungu wao ni matumbo yao. 


Wafilipi 3:17-19

[17]Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.

[18]Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;

[19]mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.

Angalia wanaokufundisha na kukuongoza, je wanaabudu nini?

Ni lazima uambiwe ukweli kwamba kufa kiroho kutakuponza. 

Mathayo 3:3

[3]Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, 

Sauti ya mtu aliaye nyikani, 

Itengenezeni njia ya Bwana, 

Yanyosheni mapito yake.

Kuwa makini tupo nyakati mbaya🤔

Mungu akubariki


Taifa Teule Ministry 

Mwl / Ev Mathayo Sudai 

0744474230 / 0628187291 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI