NITAMFANYIA MSAIDIZI…..
NITAMFANYIA MSAIDIZI.. Bwana Yesu asifiwe watoto wa MUNGU. Leo naomba tujifunze jambo moja fupi sana lenye msingi sana kwa mabinti na vijana ambao wapo katika mchakato wa kupata wenza wao wa maisha yaani kuifikia ndoa. Imekuwa kama desturi ya kila mtu mwenye uhitaji wa kuoa au kuolewa, kuwa na shauku tu ya kuangalia sifa zile anazozihitaji yeye, bila hata kujali sifa za msingi za awali ambazo kwa kuzishika hizo, mwanadamu anao uwezo wa kupata mwenza kamili kwa ajili ya maisha yake. Biblia inasema Mwanzo 2:18 “ BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu akae peke yake, NITAMFANYIA MSAIDIZI wa kufanana naye” Hapo ukipasoma vizuri utagundua kuwa Mungu kazungumza mambo machache ya muhimu sana ambayo ukiyajua yatakushindia. Karibu tuyaone. 1. SI VEMA MTU AKAE PEKE YAKE Sasa jambo la msingi hapa ni kwamba, Mungu mwenyewe anatambua kwamba, haipendezi mwanadamu akae peke yake. Maana yake suala la mtu kuwa na mwenza, ni jambo je...