BINTI ALIYEPONYWA KWA KUAMINI

       BINTI ALIYEPONYWA KWA KUAMINI


Bwana Yesu asifiwe watoto wa Mungu.

Leo naomba tujifunze jinsi imani inavyofanya kazi kwa mabinti wenye ujasiri wa kuchukua hatua katika Bwana Yesu.
 

Biblia inasema “Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma akaugusa upindo wa vazi lake. Kwa maana alisema moyoni mwake,Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. Yesu akageuka, akamwona akamwambia, jipe moyo mkuu, binti yangu; IMANI YAKO IMEKUPONYA. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.     { Mathayo 9:20-22}
 

                      Jambo la msingi ambalo kila mtu anapaswa kufahamu ni kwamba

1. Huyu mwanamke alikuwa ni mpagani kabisa mwenda kwa waganga kutafuta tiba kwa ajili ya ugonjwa wake, [Luka 8:43-44] alikuwa amemaliza mali nyingi kupeleka kwa waganga wa kienyeji kutafuta muujiza wa kuponywa.

2. Huyu mtu alikuwa ni binti, siyo mwanamke aliyeolewa na ndiyo maana ukisoma utagundua Yesu anamwita BINTI.

3 Alikuwa ni mtu ambaye ametengwa na ndugu jamaa na marafiki kwasababu ya hali yake.
 

Lakini jambo la ajabu lililomfanya binti huyu kuponywa ni IMANI yake kwa Yesu. Kitendo cha kuamini tu kwamba muujiza haupo pengine bali kwa Kristo, kilimfanya yeye Kupokea ukombozi wa tatizo lililokuwa sugu.
 

         Katika dunia hii na mazingira yetu haya, wako mabiti wengi ambao

kila siku wanaenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta mchumba,
wengine wanataka ndoa, wengine wanaenda kwa mahitaji yao
wanayoyajua wenyewe, huo ni upagani.
Pengine umeishi katika namna ya kuogopa kwamba muda
unakwenda lakini huna ndoa na huelewi nini cha kufanya, na hata
unakata tamaa. Lakini nakukumbusha leo kabla ya kukata tamaa,
hebu ikumbuke imani ya binti huyu aliyeteseka kwa miaka 12. Je
wewe umeteseka kwa habari ya ndoa kwa muda gani na huoni
majibu?. Tafakari hilo kwa makini utagundua kwamba unamwamini
Kristo au la!. Kwasababu Biblia inakiri kuwa Mwenye haki huishi kwa
imani Warumi 1:17.
Angali binti huyu, alipogundua kuwa nguvu zingine, na wataalamu
wengine hawawezi kumponya, aliipeleka imani yake yote kwa Mungu
aliye hai. Bila kujali kuwa ndugu watakuzuia, mila na desturi
zitakuzuia, marafiki watakucheka, lakii kama binti iweke imani yako
kwa Kristo yeye ndiye NURU YA ULIMWENGU.
Lakini huyu mtu alikuwa ni binti ambaye bado hajaolewa.

 Na hapa Biblia inaonyesha jinsi mabinti ambavyo huwa wanazunguka huku na
huku kutafuta msaada wa shida zao bila kujua Mungu amesema,
MSIJISUMBUE KWA NENO LOLOTE BALI KATIKA KILA JAMBO KWA
KUSALI NA KUOMBA NA KUSHUKURU, HAJA ZENU NA ZIJULIKANE
NA MUNGU, Wafilipi 4:6,

       Mabinti wengi leo hii wamejitenga na
      imani na kuanza kutangatanga hukun na kule wakidai wanatafuta
muujiza wa mchumba, jambo moja naomba likukae kichwani leo
kwamba MUNGU HUWA HATOI MCHUMBA ANATOA MUME,
kwahiyo kuwa makini na hao wachumba unaowatafuta kwa njia za mkato, usije ukapata mchumba na si mume.
 

Lakini usiogope kwamba ulishawahi kuamini mambo mengine mbali na Mungu, na hata ukatangatanga bila jibu lolote. Naomba kukukumbusha kwamba ghadhabu ya Mungu inavyokuwa nyingi kutokana na dhambi ndipo neem na rehema za Mungu zinakuwa nyingi zaidi, kwahiyo usiogope katika hali yoyote kusogea mbele za Mungu maana anahitaji kukutumia.
Kwahiyo leo jifunze kuwa na imani iliyo kuu ili Kristo akuone na kukuondolea msiba ulio nao kwani kwa Mungu, kila aaminiye hupokea, na wewe unayesoma ujumbe huu, kubali kuacha vyote unavyoviamini kuhusu unachokihitaji bali mtazame na mwamini Kristo kwa asilimia mia, ni lazima atakupa. Kwa kuamini naamuru jibu la hitaji lako likufikie KWA JINA LA YESU.
 

0628187291/0744474230

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI