BINTI ALIYEPONYWA KWA KUAMINI
BINTI ALIYEPONYWA KWA KUAMINI Bwana Yesu asifiwe watoto wa Mungu. Leo naomba tujifunze jinsi imani inavyofanya kazi kwa mabinti wenye ujasiri wa kuchukua hatua katika Bwana Yesu. Biblia inasema “Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma akaugusa upindo wa vazi lake. Kwa maana alisema moyoni mwake,Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. Yesu akageuka, akamwona akamwambia, jipe moyo mkuu, binti yangu; IMANI YAKO IMEKUPONYA. Yule mwanamke akapona tangu saa ile. { Mathayo 9:20-22} Jambo la msingi ambalo kila mtu anapaswa kufahamu ni kwamba 1. Huyu mwanamke alikuwa ni mpagani kabisa mwenda kwa waganga kutafuta tiba kwa ajili ya ugonjwa wake, [Luka 8:43-44] alikuwa amemaliza mali nyingi kupeleka kwa waganga wa kienyeji kutafuta muujiza wa kuponywa. 2. Huyu mtu alikuwa ni binti, siyo mwanamke aliyeolewa na ndiyo maana ukisoma utagundua Yesu anamwita BINTI. 3 Alikuwa ni mtu ambaye ametengwa