MAANA YA MITHALI 31:6-7
Mtu wa Mungu karibu tuchunguze majibu ya swali kutoka kwa mtumishi ignasy alilosema
SWALI: Naomba ufafanuzi kuhusu mstari wa 31:6-7 katika kitabu cha mithali.
ungana na mimi Mathayo sudai katika kujifunza jambo hili...
JIBU
Mithali 31:6-7 Biblia inasema ....''Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. Anywe akasahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
Sasa mtu wa Mungu ukianza kusoma kuanzia kifungu cha kwanza, biblia inasema...
1 Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.
2 Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?
3 Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.
4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
Utagundua kuwa mfalme lemueli anatoa maneno aliyokuwa anashauriwa na mama yake hapo mwanzo na yeye lemueli alikuja kuyatoa au kuyazungumza mahusia ya mama yake baadae.sasa kabla ya kujibu swali hilo tusome kifungu hiki cha 1 Timotheo 5:23 Biblia inasema ''Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.''
Sasa hapa paulo alikuwa anamwambia timotheo atumie pombe kidogo kwa ajili ya tumbo kama dawa, ila si kwa kulewa. kwasababu pombe ilikuwa inatumika kama dawa ya tumbo.
Hivyo tukirudi pale kwenye swali letu mstari wa sita na saba tunaona inasema ''Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea
kupotea panapozungumzwa hapo ni kufa kwa maradhi,,yaani ugonjwa . Kwahiyo ni kama mtu anayemwambia ampe dawa mtu anayeugua kiasi cha kupotea(kufa).
Shukrani bro ila nlikua na swali?
JibuFutauliza tu mtu wa Mungu hilo swali lako
Futa