JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?


         Advance 14 feb Happy Valentines Day Whatsapp Dp Images Wallpapers 2018 

                       JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

Mimi ni MATHAYO DAUDI SUDAI ambaye kwa neema ya Mungu nakuletea somo hili ambalo limekuwa ni fumbo na kitendawili kwa watu wengi

KITENDAWILI: Je! ni sahihi kwa mtu wa Mungu aliyeokoka ,kusherehekea siku ya valentine's day?

JIBU:

Valentine day ilianza katika karne ya 3,yaani mwaka 270,wakati Rumi ipo chini ya utawala wa mfalme CLAUDIUS II ambaye alikuwa ni mpagani asiye mwabudu Mungu wa kweli,JEHOVA.

Mfalme huyu alikuwa na mbinu za kuimarisha nguvu ya jeshi ambapo aliamua kutoa amri ya kwamba wanajeshi wote wa Rumi  wanapaswa wajitoe kwa ukamilifu kwa nchi yao,hivyo hawapaswi kuoa akiamini kuwa jeshi bora linajengwa na watu ambao hawajaoa, kwa kusema kwamba;endapo wakioa watakuwa na mambo mengi ya shughuli za kifamilia hivyo hawatokuwa wakakamavu zaidi katika jeshi.

Lakini padri mmoja aliyeitwa valentine [valentino] aliona jambo hilo lililowekwa na mfalme ya kwamba,si haki kwamba wanajeshi wasioe;akidai kuwa na sababu za kidini na pia amri ile inawagandamiza na kuwanyima watu haki zao.

Padri huyu wa kanisa katoliki aliyeishi katika karne ya 3 chini ya mfalme wa kipagani claudius ii alianza kufungisha ndoa kwa siri sana,jambo ambalo alikwenda kinyume na amri ya mfalme Claudia.Baadae padri huyu alijulikana na taarifa kufika hadi kwa mfalme claudius.Mfalme claudia alighadhibika kwa kuona ya kwamba yupo mtu ambaye anampinga na akaamuru akamatwe ili kuhukumiwa kifo.

Valentino alikamatwa....na wakati padri huyu yupo gerezani akisubiri hukumu,historia inasema kwamba alimpenda binti wa mkuu wa gereza ambaye alikuwa kipofu;alimuhudumia binti yule hadi alipopona  na kupata kuona tena.

Siku ya kuhukumiwa kwake ilipofika padri valentine,alimtumia mwanamke aliyempenda,barua {KADI}. ;na mwisho wake aliweka sahihi yake iliyoandikwa '' KUTOKA KWA  VALENTINE WAKO'' .na ndipo akaenda kuuawa kutokana na hukumu yake mnamo tarehe 14/02/270.

Lakini jambo la kufahamu kutoka kwenye ile kadi ni kwamba; sahihi ile haikumaanisha kwamba ni kutoka kwa valentine wako yaani mtu akupendaye bali alimaanisha kutoka kwa rafiki yake anayeitwa valentine au valentino; mfano ,padri yule angeitwa yohana basi sahihi ile ingeandikwa ,''kutoka kwa Yohana wake'' ikiwa na maana ya ''kutoka kwa rafiki yako Yohana''.

Baada ya miaka mingi kupita watu wa dunia waliichagua siku ile ya kifo cha valentine,na kuwa siku ya kupelekeana kadi za mapenzi kwa watu wanaowapenda kwa mfano wa yule padri alivyofanya  wakidai kumuenzi padri kama mtu ambaye ni mfia dini aliyekubali kufa kwa ajili ya watu kupata haki zao kwa wapenzi wao.


je kuna siri gani kati ya siku ya valentine's day  na wakristo?

katika ulimwengu wa giza,shetani ameifanya siku hii kuwa maarufu sana ulimwenguni ,akilenga kuwaangusha wale walio wa taifa la Mungu; kwasababu imekuwa ni jambo la kawaida kwamba siku hii ya valentine ni siku ambayo:

  • Watu wengi wanajihusisha na uzinzi
  • Watu wengi wanahudhuria katika kumbi za starehe 
  • Watu wengi wanajikuta katika wimbi la ulevi
  • Ndoa za watu wengi huvunjika 
  • Wengi hujikuta katika ugomvi kwa ajiri ya mapenzi.
  • Ni siku ambayo inachochea watu kufanya mapenzi,angali biblia inasema...Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini, MSIYACHOCHEE MAPENZI,WALA KUYAAMSHA, Hata yatakapoona vema yenyewe.                          (WIMBO ULIO BORA 3:5) 
Jambo la kawaida la kujiuliza ni kwamba.....kwani siku hii inakusaidia nini katika imani yako? au je ni siku ambayo inalenga kuangusha imani yako?,hatujui wala historia haijaweka wazi juu ya kile ambacho kiliendelea baada ya kifo cha valentine,inawezekanaje kwa mkristo aliyeokoka kitu asichokifahamu? ,kumbuka biblia inasema....Mimi nazichukia sikukuu zenu,nazidharau,nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini..[Amosi 5:21]. hapa ni pale wana wa israeli walipoacha njia ya Mungu na kuanza kuabudu sanamu ya ndama na miungu mingine hata kumuacha Mungu;baada ya pale walianza kufanya sherehe zisizo na maana mbele za Mungu,wala hazimtukuzi Mungu.Je kwa tabia na sifa za valentine's day zilivyo unaweza ukasema inampendeza Mungu au tunakuwa kama waasi mbele za Mungu wetu. kumbuka biblia inasema,,,Tangu sasa hivi msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu,bali katika mapenzi ya Mungu,wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi,wakiwatukana nao WATATOA HESABU KWAKE YEYE aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.[1 Petro 4:2-5]

Siri iliyojificha ni kwamba katika dunia ya leo, watu wengi hawajui kuwa valentine's day ni moja kati ya siku ambazo ni mpango na ni siku ambayo shetani anaitumia kuvuna idadi ya watu wengi na hata kuwaangusha chini.

       Hivyo kwa mtu ambaye ameokoka na ni mwana wa Mungu,HAIFAI KUIENZI NA KUISHEREKEA SIKU YA VALENTINE'S DAY.


Taifa Teule Ministry 

Mwl / Ev Mathayo Sudai 

0744474230 / 0628187291 


Maoni

  1. Ubarikiwe mtumishi wa Mungu kwa somo zuri na kutufumbua macho, kwani wakristo wengi wanasherekea hizi siku bila kujua chanzo chake ni nini na wasijue kua wana jiingiza kwenye mifumo ya shetani

    JibuFuta
    Majibu
    1. Amen ubarikiwe Sanaa mtumishi wa MUNGU azidi kukutumia na kukupa mafunuo mengi..... Mimi sikua najua kabisa

      Futa
  2. Aminaaa kwa kutumbusha lazimaaa tuhubiri kweli ya Mungu ubarikiwe Sana Mtenda KAZI wa Bwana

    JibuFuta
  3. Ameni,,chombo chaYESU

    JibuFuta
  4. 🙏🙏🙏 Mungu akubariki

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI