JE NI SAHIHI KUOA AU KUOLEWA NA MTU ULIYEMZIDI UMRI?

 Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?


Mimi ni Mathayo Daudi Sudai naomba ungana nami katika mfululizo wa masomo juu ya ndoa .
Karibu......

Je Kwa mwanaume ni sahihi kuoa mtu uliyemzidi umri?..Na kwa upande wa mwanamke ni sahihi kuolewa na mwanaume uliyemzidi umri? (kuolewa na wanaume vijana)..Je ndoa za jinsia moja ni ishara ya nini? je watu watakuwa wakioa na kuolewa katika siku za mwisho inamaanisha nini?

JIBU: Biblia haijaweka katazo lolote kwa mwanaume kuoa mwanamke aliyemzidi umri au kwa mwanamke kuolewa na mwanaume uliyemzidi umri. Lakini kilichokataza ni tamaa.

Katika hizi siku za mwisho..Biblia imetabiri kuongezeka kwa maasi..na moja ya maasi hayo ni kuongezeka kwa Tamaa..Na Tamaa kubwa inayoikabili ulimwenguni ni tama ya uasherati…nyingine ni tamaa ya mali na umaarufu. Lakini namba moja ni tamaa ya uasherati na ya mali inashika nafasi ya pili.

Nyakati hizi za mwisho biblia imetabiri kuwa watu watakuwa wakioa na kuolewa.

Luka 17:26 ”Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.

27 Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote”


Sasa kuoa au kuolewa sio kubaya…Lakini kuoa na kuolewa kunakozungumziwa hapo ambako ni kubaya na kwamba kutakuja kutokea katika siku za mwisho ni NDOA ZA JINSIA MOJA pamoja na NDOA ZA TAMAA ZA WATU KUOANA WALIOZIDIANA UMRI.

Siku hizi za mwisho ndoa za jinsia moja zinaongezeka kwa kasi hususani katika mataifa ya Magharibi hakuna tena hofu…

Kadhalika ndoa baina ya vijana wa kiume na wanawake wazee zinaongezeka kwa kasi kutokana na tamaa…wazee wanawatamani vijana na vijana wanawatamani wazee..Na hiyo ni kutokana na wanaume wazee kuwachoka wake zao walio wazee kama wao na kutamani mabinti vijana na hivyo kuwaacha wake zao na kwenda kutafuta mabinti vijana wa kuwaoa..ili watimize haja zao za tamaa za uasherati.

Vivyo hivyo wanawake wazee wanawachoka waume zao ambao ni wazee kama wao..na hivyo kuwaacha na kwenda kutafuta kuolewa na wanaume vijana kutimiza matakwa yao ya uasherati.

Kadhalika wanawake vijana wanatafuta kuolewa na wanaume wazee kwaajili ya kupata mali…Na vivyo hivyo vijana wa kiume wanatafuta kuoa wanawake wazee kwasababu ya kupata mali vile vile…Sasa machafuko kama haya ndiyo yasiyompendeza Mungu na ndiyo yaliyosababisha hata dunia ya kwanza ya akina Nuhu kugharikishwa na maji.

Hivyo kwa mtu yoyote anayetafuta kuoa au kuolewa na mtu aliyemzidi au aliye chini ya umri wake…kwa namna hiyo hapo juu..mtu huyo anafanya dhambi…Na hivyo anaangukia katika kundi la watu waovu waliotabiriwa kutokea katika siku za mwisho kwamba ‘watakuwa wakioa na kuolewa’.

Lakini kama si kwasababu hizo hapo juu bali ni kwasababu ya upendo basi sio dhambi kuoa au kuolewa na mtu aliyekuzidi umri au aliyepungufu ya umri wako..

La Muhimu na la kuzingatia ni kwamba huyo unayekwenda kumwoa au kuolewa naye..angalau asiwe rika la mwanao au la mzazi wako…Kwasababu ni ngumu sana kutokea mwanamume akampenda mtu wa rika la mama yake au bibi kizee..Wengi ni tamaa tu!..inakuwa ni roho nyingine inawasukuma kufanya hivyo..

Pia awe hana mume kabisa (yaani hajaolewa) au hajaoa..Kama alishaoa na ameachana na mwenziwe huyo hapaswi kuoa wala kuolewa..anapaswa arudiane na mkewe au mumewe. Pia awe ni mkristo, kwasababu ndoa yoyote inayohusisha watu wa imani mbili tofauti hiyo sio ndoa ya kimaandiko kabisa.

Bwana akubariki.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI