JE NI SAHIHI KUOA AU KUOLEWA NA MTU ULIYEMZIDI UMRI?
Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri? Mimi ni Mathayo Daudi Sudai naomba ungana nami katika mfululizo wa masomo juu ya ndoa . Karibu...... Je Kwa mwanaume ni sahihi kuoa mtu uliyemzidi umri?..Na kwa upande wa mwanamke ni sahihi kuolewa na mwanaume uliyemzidi umri? (kuolewa na wanaume vijana)..Je ndoa za jinsia moja ni ishara ya nini? je watu watakuwa wakioa na kuolewa katika siku za mwisho inamaanisha nini? JIBU: Biblia haijaweka katazo lolote kwa mwanaume kuoa mwanamke aliyemzidi umri au kwa mwanamke kuolewa na mwanaume uliyemzidi umri. Lakini kilichokataza ni tamaa. Katika hizi siku za mwisho..Biblia imetabiri kuongezeka kwa maasi..na moja ya maasi hayo ni kuongezeka kwa Tamaa..Na Tamaa kubwa inayoikabili ulimwenguni ni tama ya uasherati…nyingine ni tamaa ya mali na umaarufu. Lakini namba moja ni tamaa ya uasherati na ya mali inashika nafasi ya pili. Nyakati hizi za mwisho biblia imetabiri kuwa watu watakuwa wakioa na kuolewa. Luka 17:26 ” Na kama ilivyokuwa s...