USIYAKUBALI MASHTAKA YA SHETANI
USIYAKUBALI MASHTAKA YA SHETANI Na. Min Mathayo Sudai Bwana Yesu asifiwe watu wa MUNGU, leo ni siku nyingine nakukaribisha kwenye ujumbe mzuri ambao utakusaidia kusonga mbele kwa jina la Yesu….. Ni mara nyingi katika dunia hii, watu wengi wanamjua Yesu au wanaokoka baada ya kuwa wameishi kwenye dhambi kwa muda mrefu…. Sasa wanapookoka huteswa na hali zao za nyuma za yale maisha ya dhambi kwasabbau ndani ya mawazo/ akili zao huanza kujiona kana kwamba wanamaovu mengi, hawastahili kusimama mbele za Mungu na jambo hili hupelekea kuwa na wasawasi juu ya hata zile toba ambazo walifazifanya. Huanza kuwa na mashaka na hata kudhania kuwa maombi yao hayasikiki kabisa mbele za Mungu …na madhara ya jambo hilo ni kwamba WANASHINDWA KUSONGA MBELE…. Lakini ashukuriwe Mungu aliyetupa neno lake kwa kinywa cha mtume Paulo kusema hivi… WARUMI 8:1-2 1 Kwa hiyo,