Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2024

USIENDELEE KUKAA, AMKA TEMBEA MBELE

Picha
  USIENDELEE KUKAA, AMKA TEMBEA MBELE. Bwana asifiwe wana wa Mungu, nawakaribisha katika siku ya Leo katika kujifunza ... Leo natamani kusema na wewe juu ya Hali ambayo inawaua wengi pasipo wao wenyewe kujua na wamebaki kuishi katika Masha ambayo hayako vizuri huku wao wakiwa ni mashahidi wa ubovu wa maisha Yao.... jambo hili huwa linaanzia pale mtu anapoanguka, dhambini au mambo Yale kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.... watu wengine wakianguka dhambini huwa wanakata tamaa moja kwa moja, 👉Kama walikuwa wanahuduma, wanaiacha kabisa 👉Kama walikuwa wanaenda kanisani, ghafla waaacha 👉Kama walikuwa wanaomba basi utakuta hawapmbi Tena kwasababu wanajisikia wakavu kabisa.. 👉Kama walikuwa na ratiba za ibada nyumbani, au ratiba za mambo ya kimungu kama semina, mikesha, kufunga,n.k basi wanajikuta wanaacha... SASA, Hapa ni lazima ujue sababu ya wao kushindwa kweda mbele ni MASHTAKA KUTOKA KWA SHETANI..., kwasababu SHETANI ndiye mshitaki na si Mungu... 1 Petro 5:8 [8]Mwe na kiasi na ku...