BUSARA ITAKULINDA...
BUSARA ITAKULINDA.... Bwana Yesu asifiwe Wana wa Mungu, ni siku nyingine, karibu tujifunze jambo la msingi linalohusu BUSARA... Mithali 22:3 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. 👉unapokuwa na BUSARA maana yake unakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.... 👉unakuwa na uwezo wa kuamua lililojema kwenye maisha yako bila kujali linaumiza kiasi gani katika maisha ya kawaida Biblia inaweka wazi kwamba Watu wanaweza kuona jambo fulani baya ambalo limetokea au linataka kutokea... Sasa, ukiwa na BUSARA maana yake ni lazima ujitenge na hayo mabaya kwa njia ya kujificha mbali nayo... Biblia inaposema kujificha... maana yake kufanya Jambo au kusimama katika mahali ambapo baya hili halikupati... 👉unapoona Kuna watu wanafanya mabaya yenye madhara, na wewe ukaamua kutembea mbali nao ili madhara hayo yasikupate hapo unakuwa umejificha 👉unapoona Kuna madhara ya uovu yanakuja kuwapata watu, halafu ukaamua kukaa mbali na uovu hapo umej