NANI YUKO NYUMA YAKO
NANI YUKO NYUMA YAKO by Min. Mathayo Sudai Bwana asifiwe... Tumshukuru Mungu kwasababu tupo salama... Tujifunze kitu hapa 👇 Kuna njia nyingi sana ambazo watu huzitumia pale wanapokuwa katika utafutaji mbalimbali... 👉Kuna wanaowategemea watu 👉Kuna watu wanategemea mali zao 👉Kuna watu wanategemea waganga na wachawi kila mtu na namna yake... 👉Kuna wengine wanamtegemea Mungu 👉na Kuna wengine wanategemea akili zao tu hizo zote ni nguvu ambazo zipo nyuma ya watu ambao wanatafuta au kuchakalika katika maisha Yao... lakini Soma hapa👇 Mithali 23:4 [4]Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe. Biblia inaposema usijitaabishe, haina maana kwamba usifanye kazi, au usitafute kazi.... lakini kujitaabisha panapozungumzwa hapo ni kule mtu kujiwekea nguvu kutoka kwa watu au kutumia nguvu zake tu ili kufanikisha Jambo... lazima ujue kwamba kutenda jambo kwa namna hiyo hakuleti mafanikio... kwasababu, ... kama mkristo unatambua kwamba tunapokuwa tuna...