Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2023

JE WAFILIPI 2:3 INA MAANA GANI

JE WAFILIPI 2:3 INA MAANA GANI ? Bwana Yesu asifiwe Wana na Binti za MUNGU. leo Ni siku nyingine tutaiangalia ujumbe ndani ya kitabu Cha Wafilipi 2:3 Wafilipi 2:3-5 [3]Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. hapo Kuna mambo kadhaa ambayo hatupaswi kuyashika pale ambapo tutakuwa tunaendenda katika Utendaji kazi wetu.. Biblia imesema tusifanye Neno LOLOTE kwa  1: KUSHINDANA     Hapa Biblia inalenga kutufanya tusiwe watu wa kufanya Mambo kujionyesha kana kwamba sisi Ni Bora kuliko watu wengine katika hali ya UBINAFSI..usifanye Jambo kwa kupambana na mwenzako huku ukimuonea wivu... ...wivu ndiyo hufanya watu kufanya jambo kwa mashindano mioyoni mwao huku wakitamani wao ndo waonekane na kusifiwa mbele ya kanisa kuliko wenzao.... 👉ukiwa na tabia ya KUSHINDANA kwa UBINAFSI ndani ya Ufalme wa MUNGU Basi jua haikubaliki kabisa ndani ya Ufalme wa MUNGU 👉Mungu anataka watu tushirikiane...