Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2023

JE UNAPENDEZWA NA MATENDO YA MUNGU

Picha
  JE UNAPENDEZWA NA MATENDO YA MUNGU Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu Leo ni siku nyingine, karibu tutazame jinsi matendo ya Mungu yanavyomfunua mtu wake. Zaburi 111:2 [2]Matendo ya BWANA ni makuu,  Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo. Anasema kuwa matendo ya Mungu ni makuu, 🙁 NA jambo kama hilo ni dhahiri kwamba kila mtu analifahamu vizuri 👉Kila MKRISTO, ukimuuliza habari za Mungu na matendo yake, anaweza akaanza kukusimulia kuanzia Mungu kuwatoa wana wa Israeli Misri mpaka walipoingia katika nchi ya ahadi. 👉Atakwambia kuhusu habari za nyoka wa shaba 👉Atakwambia habari za chakula cha mana n.k NA kimsingi mambo hayo watu huyajua toka wanavyokuwa watoto wadogo kwenye shule za watoto ( Sunday school ) Lakini hayo yote hayafunui upendo wa mtu kwa Mungu, wala hayaonyeshi mahusiano ya mtu na Mungu. Biblia inasema WANAOPENDEZWA na matendo makuu ya Mungu, huwa na muda wa kuyatafakari, kuyafikiria sana Yale ambayo Mungu huyafanya na zaidi ya yote katika kuyafikiria hayo huishia ka...