Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2023

USIPENDE KUWA MFU

Picha
  USIPENDE KUWA MFU Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, karibuni katika kujifunza ujumbe huu wenye hitaji la kukuimarisha katika pendo la Yesu na imani tuliyoachiwa kwa uweza wa Roho mtakatifu.    Mfu ni mtu au mnyama asiyekuwa na uhai.  Kitu au mtu anapokuwa katika hali ya kufa huwa anakuwa na sifa zifuatazo 👉Haoni chochote 👉Hasikii neno lolote  👉Hatambui kitu 👉Haongei kitu 👉Hawezi kufanya kazi yoyote ile.  Sasa Paulo aliwaambia waefeso kuwa hata wao walikuwa na hali hiyo.  Soma hapa👇 Waefeso 2:1-3 [1]Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; [2]ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; [3]ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Alitoa sababu ya mtu kuwa mfu, na unaposoma vizuri unag...