NINI MAANA YA KUTOKA KATIKA MADHEHEBU?
NINI MAANA YA KUTOKA KATIKA MADHEHEBU? Mimi ni Mathayo Sudai, karibu tujifunze jambo hapa leo. Kwanza jambo la kufahamu ni kwamba kila mkristo anapaswa awe na Roho Mtakatifu, ambaye kwa huyo biblia inasema ATATUONGOZA NA KUTUTIA KATIKA KWELI YOTE. Yohana 16: 13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake ”. Hivyo mtu yeyote asiyekuwa na Roho wa Mungu biblia inasema huyo si wake (Warumi 8:9) , Haiwezekani kumjua Mungu kwa namna yoyote ile,. Sasa tatizo linatokea ni pale unakuta watu wengi walipokea kweli Roho Mtakatifu mwanzoni walipoamini, lakini ilifikia wakati Fulani wakamzimisha pasipo hata wao kujijua, Uthibitisho ni kwamba utasikia mtu anakwambia mwanzoni nilipompa Bwana maisha yangu nilikuwa ni moto sana, lakini siku hizi nimepoa, ile nguvu ya mwanzo sina..sasa...