JE NI DHAMBI KULA NYAMA SIKU YA IJUMAA KUU
NI DHAMBI K ULA NYAMA SIKU YA IJUMAA KUU ? Mimi ni Mathayo Sudai. Ungana nami katika uchambuzi huu wa mapokeo ya ijumaa kuu. Ili iwe vyepesi kwetu kulielewa vizuri somo hili. Tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele viwili. Ambavyo ni:- 1.KWANINI WAKATOLIKI HAWALI NYAMA SIKU YA IJUMAA KUU? 2.UCHAMBUZI WA HOJA 4 KI-BIBLIA KUHUSU MAPOKEO YA KANISA CATHOLIC. UTANGULIZI Leo ni siku ya Ijumaa Kuu. Inaitwa siku ya ijumaa kuu kwa sababu ndiyo siku ambayo Wakristo wote kote duniani wanaadhimisha kumbukumbu ya mateso na kifo cha Yesu Kristo msalabani kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu mzima. Utasikia kwenye vyombo vya habari eti wanasema:- "......Wakristo leo wanakumbuka mateso ya Yesu kristo mwokozi wao........ Wakristo wanasherekea kufufuka kwa Yesu mwokozi wao......................................" Matamshi hayo ndani yake yamefichwa na hila fulani za shetani. Ni muhimu kuelewa vizuri hapa, Yesu Kristo hakuteseka na kufa tu kwa ajili ya wakristo wala yeye sio