JE ASIYE NA UBATIZO SAHIHI HANA ROHO MTAKATIFU?
SWALI NI Je kama hujabatizwa ubatizo sahihi huwezi kuwa na roho mtakatifu? Mpendwa,ungana nami tujifunze juu ya swali hili. mimi ni MATHAYO SUDAI karibu...... Utendaji kazi wa Roho Mtakatifu ni kama ufuatavyo, Mungu anapomchagua mtu aliye dhambini, huwa anamtumia Roho wake mtakatifu kumvuta mtu yule ndio hapo mtu huyo anaanza kusikia kuhukumiwa dhambi zake moyoni, na hatimaye anafikia toba, sasa huyo ni Roho Mtakatifu siku hizo zote anakuwa anamvuta mtu yule, anakuwa anatembea na yule mtu kama rafiki yake wa pembeni, lakini bado hajaingia ndani yake, ni kama mwanamume anapokuwa katika hatua za awali za kumchumbia mwanamke, anakuwa anaweza kuwa karibu naye, kumpa zawadi chache chache, kuzungumza naye maneno mazuri, kumwonyesha vitu vyake n.k, hayo yote mwanamume anayafanya ili tu kumvuta yule mwanamke, lakini bado yule mwanamke sio mali yake mpaka siku atakayoamua kumkubalia na kufunga naye ndoa, ndipo siku hiyo atakuwa milki halali ya yule mwanamume. ...